RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA ALIYEKUWA RAIS WA BURUNDI PIERRE NKURUNZINZA.

 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya  Kikwete aomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Marehemu Pierre Nkurunzinza kwa kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Burundi jana jijini Dar es Salaam.  Dkt. Kikwete amefahamiana na Marehemu Pierre Nkurunzinza kwa zaidi ya miaka 20 tangu wakati wa mazungumzo ya amani ya Burundi wakati huo Rais Kikwete akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Rais Nkurinzinza akiwa kiongozi wa CNDD-FDD na baadae wote wakiwa Marais wa nchi zao.

No comments: