RAIS MAGUFULI ATUMA UJUMBE MZITO KWA VIONGOZI WA SERIKALI WANAOTAKA KUGOMBEA UBUNGE WAKIDHANI WATAKUWA MAWAZIRI



Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS Dk.John Magufuli amepeleka salamu kwa baadhi ya viongozi wa kada mbalimbali wanaodhani wakiachana nafasi zao na kwenda kugombea ubunge wakishinda atawateuwa katika Baraza la Mawaziri wajue wanajidanganya.

Ameyasema hayo leo Juni 22,2020 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta , Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele ,Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa,Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima pamoja na Mkurugenzi wa Kaulia Jerry Pima.

Rais Magufuli amesema kwenye siasa yanazungumzwa mengi lakini ametoa mwito kwa viongozi anawaoteua waridhike na nafasi walizonazo.
"IGP Sirro nitashangaa sana akitoka hapa na kwenda kugombea ubunge Bunda akidhani akiwa mbunge atakuwa Waziri, Hivi kama nataka uwe Waziri nitakuteua kuwa mbunge na kukupa uwaziri.
 
Hata ukienda jimbo ukashinda bado sitakupa uwaziri, "Watu hawalewi historia ,kuna mtu nadhani ni Dk.Ndumbaro tulimteua ubunge Songea Mjini alikuwa nafasi ya tatu kwenye kura za maoni lakini tukamchukua na kuacha wengine walioongoza .

"Huyu Dk.Ndumbaro sasa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje.Je hao wenye kutumaini uwaziri wanauhakika gani kama watapita na nitawachagua kuwa mawaziri , kwanza itategemea na siku hiyo nimeamkaje,"amesema Rais.

Ameendelea kueleza kuwa atashangaa iwapo Mkuu wa Majeshi ataenda kugombea ubunge akidhani atamchagua kuwa Waziri wa Ulinzi."Nitamshangaa, kweli demokrasia ni pana kama unaamini utashinda nenda .

"Najua wewe Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.Jon Pima ulikuwa na mawazo ya kutaka kwenda kumtoa Msukuma, ukitaka kwnda nenda. Lakini niwaombe mfikirie zaidi, kama unajukumu lako kubwa unalifanya vizuri na watu wanakuamini, basi litumikie hilo .

"Nikushangaa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro uwe na mawazo ya kwenda Monduli kugombea ubunge, lakini ndio demokrasia, lakini najua kuna viongozi wengi wazuri wanafanya kazi zao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli

No comments: