RAIS JPM ATEKELEZA AHADI YA KUJENGA DARAJA LA MTO SIBITI MKOANI SINGIDA ALILOAHIDI MWAKA 2015
Na Jumbe Ismailly- MKALAMA
WANANCHI wa Kata ya Msingi,pamoja na vijiji vinavyozunguka kata hiyo wilayani Mkalama,Mkoani Singida wataondokana na adha ya kutokwenda kwenye huduma za afya,elimu pamoja na kusafiri kwenda kwenye masoko ya mazao wanayozalisha mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja la mto Msingi.
Ujenzi wa daraja hilo ulioanza kujengwa juni,11,mwaka jana kwa mkataba wa miezi 24 ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa kampeni za kuomba kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo,kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi,Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Singida,Mhandisi Matari Masige alisema kwamba ujenzi wa daraja la msingi utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 9.02 unatarajia kukamilika mwaka ujao.
“Ilikuwa mwaka 2015 Mheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa anaomba kura alipofika eneo hili daraja lilikuwa limezuia magari kupita kwa sababu lilikuwa limetitia,kwa hiyo wananchi wakamwambia Mheshimiwa kama unataka kura za huku tujengee daraja la kudumu.”alibainisha Kaimu Meneja huyo.
Hata hivyo Mhandisi Masige alisisitiza pia kwamba kimsingi daraja la msingi pamoja na ahadi aliyotoa Rais wakati wa kampeni,lakini dhumuni lake kubwa ni kuunganisha Mkoa wa Singida pamoja na mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni Simiyu na Mara kupitia daraja la mto Sibiti.
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja huyo wa TANROADS Mkoa wa Singida shilingi milioni 14 zilitumika kuwalipa wananchi fidia waliokuwa wakiishi kuzunguka daraja hilo na hakuna mwananchi aliyelalamika kuhusu malipo hayo ya fidia.
“Kama mnavyofahamu daraja la Sibiti sasa limeshakamilika magari yanapita juu kwa hiyo kukamilika kwa daraja hili pamoja na daraja la Sibiti ambalo limekamilika Mkoa wa Singida utakuwa umeshafunguka kwa asilimia mia moja.”alisisitiza kaimu meneja huyo.
Kwa mujibu wa Mhandisi Masige daraja hilo litakalojengwa kwa zege litakuwa na ukubwa wa mita 75 litakapokamilika na gharama za mradi huo itakuwa zaidi ya shilingi bilioni 9.02 na fedha zote hizo zinatolewa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na hakuna hata senti moja iliyotolewa na wafadhili.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa muda wa ujenzi wa daraja hili ni miezi 24 na mpaka ninavyoongea sasa hivi,nilisaini tarehe 11,05,mwaka 2019 mpaka sasa tumeshamaliza miezi 12 lakini maendeleo ya mradi ni mazuri.”alisema kaimu meneja huyo wa Tanroads.
Aidha Mhandisi Masige alisisitiza pia kwamba mpaka sasa Mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo ameshalipwa zaidi ya shilingi bilioni 2.85 na kwamba pamoja na kiasi hicho cha fedha kuna zaidi ya shilingi bilioni 1.35 kama malipo ya awali na wakati wowote wanatarajia kumlipa zaidi ya shilingi bilioni 1. 286.
Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi alisema kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutawahamasisha wananchi kuzalisha bidhaa ambazo soko lake halipatikani ndani tu ya nchi bali watazalisha bidhaa ambazo soko lake linapatikana hata nje ya Tanzania.
Aidha Dkt Nchimbi aliweka bayana kwamba awali inawezekana wananchi walikuwa wanakata tamaa ya kufuga mifugo kwa kuwa walikuwa hawalioni soko la mifugo yao,lakini sasa kutokana na kukamilika kwa daraja hilo watafuga mifugo na katika ubora unaotakiwa kwa sababu soko la uhakika la mifugo yao,hususani nyama na mazao mengine ya mifugo halitakuwa ndani ya nchi tu.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Msingi,Basili Salehe Kayombo aliweka bayana kuwa kukamnilika kwa daraja hilo litawarahisishia wakulima kusafirisha mazao yao kupeleka kwenye masoko ya mazao,kwanza hiyo barabara ndiyo barabara kuu inayounganisha na barabara ya Mwanza kuingia Singda.
“Hili daraja ambao lipo changamoto ilikuwepo kwamba liliwahi kukatika na kusababisha wananchi wa maeneo hayo kukosa huduma za kuvuka kwenda wilayani Iramba ambako kuna huduma muhimu za kijamii.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt. Rehema Nchimbi yupo katika ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maeendeleo iliyopo katika Halmashauri zote za Mkoa huo kuanzia Juni,10 hadi juni,18,mwaka huu kujiridhisha matumizi ya fedha za serikali.
Mafundi wa ujenzi wakiendelea kufanyakazi ya kujenga daraja la mto Msingi lililokuwa limeharibika kwa kipindi kirefu na hivyo kusababisha wananchi kuksa huduma za kijamii kwenye maeneo zinakopatikana huduma hizo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
Ni baadhi ya watumishi wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida kabla ya kuanza kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la mto Msingi,wilayani Mkalama,Mkoani Singida alipokuwa kwenye ziara ya siku moja wilayani hapa.
Ni barabara iliyopo kwenye daraja la mto Msingi inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami ili kuliimarisha daraja hilo.
Ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt.Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akitembelea kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la mto Msingi,ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiomba kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Ni barabara iliyopo kwenye daraja la mto Msingi inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami ili kuliimarisha daraja hilo.
Ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt.Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akitembelea kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la mto Msingi,ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiomba kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
No comments: