KHERI JAMES AIPASUA NGOME YA CHADEMA ROMBO.



************************************
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Komred Kheri James amepasua ngome ya Upinzania katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro kwa Kupokea Viongozi mbalimbali wa Chama Hicho.
Viongozi walio pokelewa leo ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Rombo ndg Athuman Mohammed Kimario ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rombo Evarist Silayo Mgoyoni,na Madiwani Simon Peter Marandu kata ya Mrire,Justina Maliangu Mkenda kata kisale,Paul Adelaro ulimalya kata ya Aleni,Nicholaus Kimario kata ya kitongo wamejiunga na Chama cha Mapinduzi CCM muda huu katika ziara ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri Denice James inayoendelea Wilayani humo muda huu.

No comments: