JESHI LA POLISI KUANZA KUTUMIA JENGO LA MAKAO MAKUU DODOMA MWISHO WA MWEZI
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, ametembelea na kukagua maendeleo na marekebisho ya jengo ambalo lilikabidhiwa kwa Jeshi la Polisi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli,.
Katika ukaguzi huo, IGP Sirro, ameelekeza kukamilishwa kwa ghorofa ya pili na ya tatu ambayo inakisiwa kugharimu kati ya shilingi milioni 150 hadi milioni 200 tayari kwa matumizi ya maafisa na askari ambao wanatarajiwa kuwasili jijini Dodoma mwishoni mwa mwezi huu.
IGP Sirro amesema hayo leo akiwa akiwa jijini Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akipata maelezo alipotembelea na kukagua maendeleo na marekebisho ya jengo la Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dodoma, ambalo lilikabidhiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akikagua maendeleo na marekebisho ya jengo la Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dodoma,
No comments: