DKT MLIMUKA AONGOZA UZINDUZI WA MWONGOZO WA KAZI KWA NCHI ZA SADC KUPITIA JUKWAA LA SEKTA BINAFSI SPSF
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Jukwaa la Sekta binafsi SADC (SPSF) imezindua Sheria za Kazi za SADC ikijumuisha sera, vipaumbele, maswala, na mipango kwa wafanyakazi wa sekta binafsi.
SPSF kwa msaada wa Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO), waliweza kutunga mwongozo wa Sheria ya Kazi katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.
Uzinduzi wa mwongozo huo wa sheria ni kwa lengo la ufikiaji kwa sheria za kazi kwa nchi zote 16 za Ukanda wa Kusini mwa jangwa la sahara SADC kwa kufuata wajibu wa kisheria kwa waajiri, kuwa na kanuni nzuri za Kazi, kuboresha, kufuata, na kuwezesha biashara na ajira ndani na kati ya nchi za SADC.
Akizungumzia uzinduzi huo, Mwenyekiti wa SPSF Dkt Agrrey Mlimuka amesema wamefurahi kuona sheria za kazi katika.nchi 16 za SADC zinafanana kwa kiasi chake na hata pia zimeonesha njia nzuri hata kwa wafanyabiashara wanaotaka.
Amesema, mwongozo wa sheria za kazi ni wa kuvutia, na unaruhusu maendeleo na ukuaji endelevu katika bara hili kwani itawezesha mtiririko wa uwekezaji katika nchi zetu.
Dkt Mlimuka amesema, Mwongozo wa Sheria ya Kazi imekaribisha ushindani na pia imeangalia upatikanaji wa vibali vya kazi kwa wafanyakazi wanaotoka katika nchi za ukanda wa SADC, maslahi ya kazi na mambo muhimu kwa mwajiriwa.
SPSF ni sauti inayounganisha nchi 16 za SADC katika sekta binafsi juu ya sera za nchi za ajira, vipaumbele, maslahi ya waajiriwa, kupata vibali vya kazi kwa mwajiriwa au mfanyabiashara na vitu vingine muhimu.
Aidha, jukwaa hilo pia limeweza kujumuisha majadiliano juu ya Mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 unaosambazwa na Virusi vya Corona wakiweka vidokezo muhimu vya udhibiti ikiwemo bidhaa kupitia bandari.
No comments: