ZALISHENI KWA WINGI ILI WATANZANIA WAMUDU BEI YA BIDHAA ZA MAPAMBANO YA COVID 19 RAS ARUSHA
Karibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiwa na Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt.Edson Sichalwe wakiwa na Meneja wa Sido Mkoa wa Arusha Nina Nchimbi pamoja na Mwenyekiti wa wajasiriamali wadogo wa Sido Mkoa Yasin Bakary wakati wa utambukishaji wa bidhaa zao kwa ajili ya mapambano ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhiwa vifaa tiba vya kupambana na maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 kutoka kwa wajasiriamali wa mkoa wa Arusha ambao wameenza kutengeneza bidhaa hizo ikiwemo Sabuni za maji Vitakasa mikono pamoja na Barakoa kwenye eneo la Sido Mkoa wa Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Mwenyekiti wa wajasiriamali wa mkoa wa Arusha ambao wapo chini ya shirika la kusaidia viwanda vidogo Sido Yasin Bakary akimkabidhi Katibu Tawala Richard Kwitega Lita Tano za kitakasa mikono pamoja na Sabuni kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo
Mganga Mkuu wa Mkoa huo Edson Sichalwe akiongea na kuwataka wajasiriamali na wadau wengine kuendelea kupambana na Ugonjwa huo kwa kushirikiana na serikali kuwasaidia wananchi kupata bidhaa za kujikinga na maambukizi kwa bei wanazomudu.
Sehemu ya wajasiriamali wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa kinga kwa ajili ya kuendeleza Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 .
Meneja wa shirika la viwanda vidogo vidogo Sido Mkoa wa Arusha Nina Nchimbi akiongea na vyombo vya habari hawapo pichani mara baada ya wajasiriamali kukabidhi vifaa kinga vya Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 leo jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Sehemu ya bidhaa za Wajasiriamali waliochini ya Sido Mkoa wa Arusha ambazo ni Sabuni ya Maji Vitakasa mikono Pamoja na Barakoa kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Covid 19 zinazotengenezwa hapa nchini na kuuzwa kwa bei rafiki kwa watanzania
Wajasiriamali wakiwa na Karibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega mara baada ya kumkabidhi virltakasa mikono Sabuni na Barakoa ambazo wanatengeneza na kuuza kwa bei ya kati ya 700 kwa Barakoa huku kitakasa mikono 2000 kwa ujazo wa mml.60 kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa kinga vya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 leo jijini Arusha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Karibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega ameyataka makampuni viwanda na wajasiriamali wenye viwanda vidogo vidogo kugeukia kuzalisha kwa wingi na kutengeneza vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid unaosababishwa na virusi vya korona ili wananchi wapate bidhaa hizo kwa bei inayoendana na uhalisia wa maisha ya mtanzania.
Kwa muktadha huo akawataka wajasiriamali wa mkoa wa Arusha chini ya Sido kutumia malighafi zetu za ndani na utaalamu wetu wa ndani katika kupambana na maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 unasababishwa na virusi vya korona kwa kuwa janga hili linatupa ya Sote
Kwitega aliyasema hayo wakati akipokea vitakasa mikono sabuni na barakoa zilizotengenezwa na wajasiriamali wa mkoa wa Arusha wanaofanyakazi chini ya Sido kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Alisema kwa wajasiriamali hao wameonyesha muitikio wa kauli ya mh.Rais wa kutumia ubunifu wetu wa ndani wa kutengeneza bidhaa zao kwa kutumia malighafi zetu za ndani kuwezesha watanzania kuweza kujikinga na Ugonjwa wa Covid 19 bila kutumia gharama kubwa ya kununua bidhaa hizo.
"Mmetuonyesha kwa vitendo kuwa bidhaa hizi ambazo zinauzwa kwa bei elekezi ya serikali kwa ujazo wa mml40 kwa bei ya tsh.2000 badala ya tshs.3000 jambo hilo litasaidia watanzania wengi kuweza kujikinga na Ugonjwa huu"alisema Kwitega
Kwa Upande wake Meneja wa Sido Mkoa wa Arusha Nina Nchimbi alisema kuwa baada ya janga hili kutokea tuliona ni fursa kwa wajasiriamali kuweza kuzalisha bidhaa zenye viwango vinavyokubalika ili kuokoa watanzania na janga hili ndio maana leo tupo hapa kutambulisha bidhaa hizi.
Alisema kuwa Sido siku zote ipo kuwaonyesha njia wajasiriamali katika kutengeneza bidhaa zenye ubora unaokubalika sanjari na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zinapingana na maisha ya Mtanzania.
Awali akitoa taarifa mbele ya Karibu tawala wa mkoa wa Arusha Mwenyekiti wa Wajasiriamali waliochini ya Sido Yasin Bakary alisema bidhaa hizo ikiwemo Sabuni za maji Vitakasa mikono na Barakoa wanauza kwa bei inayowajali watanzania ikiwemo Barakoa kwa tshs.700 badala ya 3000 au 1000.
Alisema walipoona bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi zimekuwa bei juu waliamua na kuona watumie bidhaa za ndani kuzalisha bidhaa za kujikinga na Ugonjwa wa Covid 19 ili kuwasaidia watanzania kwenye mapambano ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa homa kali ya mapafu.
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt.Edson Sichalwe alisema kuwa wamejikita kutoa elimu kwa jamii kujikinga na Ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid 19 na kwa sasa wamejikita kwenye uvaaji wa barakoa
Akawataka kuunganisha nguvu kwani mapambano ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Covid 19 si ya wizara ya Afya pekee ni kwa kila mdau kushiriki ikiwemo hili la uzalishaji wa bidhaa za kujikinga kwa kuzalisha kwa wingi ili kumfikia mwananchi wa chini kwa bei ya chini anayoweza kuimudu.
No comments: