WATUMIAJI WA TECNO CAMON 15 WAFUNGUKA

IKIWA ni takriban mwezi mmoja umepita tangu kampuni ya simu za mkononi ya TECNO kuzindua simu yake mpya CAMON 15 kwa njia ya mtandao, watumiaji wengi wa simu hiyo wameeleza namna simu hiyo ya CAMON 15 ilivyo na utofauti na simu za makampuni mengine na matoleo yake yaliyopita.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maduka ya TECNO kuhusu simu hiyo, watumiaji hao wamekiri kuwa CAMON 15 imekata kiu yao ya kile walichokuwa wanakihitaji siku zote kutokana na kuridhishwa na ufanisi wa mifumo endeshi ya simu hiyo pamoja na sifa nyinginezo.
Marceline John (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya begi na msimamizi wa duka la TECNO.

“Hii simu ni moto mwingine kabisa, ni simu ambayo sijutii kununua na hapa naona pesa yangu imeenda kihalali yaani. Binafsi kinachonifurahisha sana ni mwonekano wa simu, kamera na betri” Alisema Bi. Marceline.

Kwa upande wa watumiaji wengine wameelezea kuhusu CAMON 15 kuwa imewaondolea kikwazo cha kupiga picha nyakati za usiku na sasa wanaweza kupiga picha wakati wowote na mahali popote.

“Simu hii ya CAMON 15 imemaliza kabisa tatizo la kupiga picha usiku, unajua sisi wengine ni watu wa harakati nyingi sasa unapokuwa na simu kama hii picha unachukua freshi kabisa usiku na inatoka vizuri sana” Alisema Rajab Said.
Rajab Said Mteja wa TECNO CAMON 15

TECNO ambayo ni kampuni ya simu kinara wa simu janja Tanzania imeshauza simu yake hii mpya CAMON 15 zaidi ya simu 2500 ndani ya mwezi mmoja tangu ilipozinduliwa katikati ya Aprili 2020. Mpaka sasa CAMON 15 inapatikana nchi nzima yakiwemo maduka makubwa ya TECNO na maduka ya wauzaji wa simu nchini kote. 
Shamimu Ramadhani (kushoto) na Veronica Swai (kulia) wakikabidhiwa zawadi na msimamizi wa duka la TECNO (Katikati) baada ya kununua TECNO CAMON 15.

No comments: