WAFAHAMU WAHALIFU WALIOVUNJA REKODI YA KUMILIKI MAMILIONI YA PESA DUNIANI


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

LINAPOKUJA suala la kutengeneza fedha sio kila mtu atatengeneza fedha kwa njia halali, baadhi ya wahalifu ulimwenguni wamefahamika zaidi kutokana na umiliki wao wa pesa nyingi zilizopatikana kwa njia isiyo ya halali, wengi wao wamekuwa wakipata pesa kupitia biashara haramu ikiwemo uuzaji wa dawa za kulevya, kuendesha mitandao ya ngono, uuzaji wa binadamu, ujangili na hata kutumia silaha ili kujipatia mali.

Licha ya shughuli zao kuwaweka katika hatari kubwa baadhi ya wahalifu wameweza kutengeneza kiasi kikubwa cha fedha ingawa hawawezi kufurahia fedha hizo kwa uhuru ukilinganisha na wananchi wa kawaida.

Baadhi ya wahalifu waliotengeneza kiasi kikubwa cha fedha ni pamoja na;

Carlos Enrique Lehder Rivas (dola bilioni 2.7)

Ni mwanzilishi mwenza genge la dawa la kulevya la Medellian Cartel na alianza kazi ya uhalifu kwa kuuza magari ya wizi, bangi na mwishowe Cocaine pia alisimamia vikosi vya genge vya wamiliki bunduki, boti, helikopta, mashamba ya mbio za farasi na kundi lake la Neo-Facist.

Alikamtwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha bila msamaha na miaka 135 ambayo ilipunguzwa hadi kufikia 55 na bado yupo chini ya uangalizi huko Marekani.


Khun Sa (dola bilioni 5)

Kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 Khun alijulikana sana kama mpenda dawa wa kulevya na mwongozaji magenge ya uharifu, alifanya biashara ya silaha ili kujipatia ulinzi.

Mwaka1996 alijisalimisha katika Mamlaka za ulinzi huko Burma kwa sharti la kupewa ulinzi toka kwa Serikali na mwaka 2007 akiwa na miaka 73 alifariki dunia kwa sababu zisizoeleweka.

Viktor Bout (dola bilioni 6)

Bout alishtakiwa kwa tuhuma za mauaji dhidi ya maafisa wa Marekani,. Kushirikiana na kundi la ugaidi la FARC, udanganyifu pamoja na utakatishaji fedha ili akuze biashara yake, mwaka 2012 alihukumiwa kifungo cha miaka 25.


Amado Carillo Fuentes ( Dola milioni 25)

Huyu anatajwa kuwa tajiri wa pili katika genge la wauza dawa za kulevya, amekuwa akisambaza dawa hizo katika mataifa ya Marekani, Mexico na Columbia, alifariki mwaka 1997 baada ya upasuaji wa kubadili mwonekano wake kushindikana na baadaye daktari aliyefanya upasuaji huo alikutwa amekufa huku akiwa amefungwa katika chuma na ilielezwa kuwa aliteswa kabla ya kuuwawa.

Pablo Emilio Escobar (Dola bilioni 30)

Anafahamika zaidi kwa jina la "Father of Cocaine" akiwa na miaka 35 alikuwa mmoja wa watu watajiri zaidi duniani, licha ya kutofahamika kwa kiasi alichokitengeneza inakaridiwa alikuwa na umiliki wa dola za kimarekani bilioni 30, imeelezwa kuwa Pablo amekuwa akisambaza asilimia 80 ya dawa za kulevya nchini Marekani katika miaka ya 80 huku ikikadiriwa alikuwa akitengeneza dola za kimarekani 420 kwa wiki, alifariki mwaka 1993.

No comments: