TAURUS MUSIK WATAMBULISHA WASANII WAKE WAPYA 'KEEMLYF', 'TALLIE'

NA ANDREW CHALE

LEBO ya muziki ya Taurus 'Taurus Musik'  yenye makao makuu yake nchini Kenya, imetambulisha rasmi Wasanii wake wawili wapya sambamba na nyimbo zao mpya ambazo kwa sasa zimekuwa gumzo Ukanda wa Afrika Mashariki.

Kiongozi wa Lebo hiyo, Issa Arafat amewataja Wasanii hao ni pamoja na Omambia Nelson Asaeli 'Keemlyf' na  mwanadada Tali Khasoah Linnet ama 'Tallie'.

Keemlyf na Tallie tayari wameachia kazi zao za kwanza video chini ya lebo hiyo zilizoongozwa na 'Director' Trey Juelz wa Taurus Muzik.

Upande wa Keemlyf ama 'One Man Killer' ametoa wimbo wa 'Pita na Wewe'  ucheki hapa👉 https://youtu.be/B4cUtoNA9Ds

Kwa sasa Keemlyf ni miongoni mwa vijana wenye vipaji nchini kenya ambapo amekuwa na aina yake ya muziki.

"Keemlyf anatumia 'style ' yake na ya kipekee katika muzuki wake. Tumeona wimbo wake wa Banana namna ulivyomuweka kayila ramani ya muziki na kutikisa kwenye televisheni, radio na mitandaoni.

Kwa sasa tunahakika kuwepo kwake na Taurus muzik atakuwa bora zaidi na kufika mbali" ulisema Arafat.

Kwa upande wa Mwanadada Tallie  yeye ameachia wimbo wake mpya kwa jina 'Bugia'. Unaweza kuutazama hapa👉 https://youtu.be/hCm5cUqbTnQ

Tallie ni msanii mpya na anayechipukia ambapo alisaini katika lebo hiyo tangu 2019 na kupikwa kipaji chake.

"Tangu kujiunga kwake na Taurus Musik, ameibua matumaini makubwa na jamii inashauku kubwa ya kupokea kazi zake.

kwa sasa tuipokee rasmi 'Bugia'  ambayo inakuja kubamba Afrika Mashariki". Alisema Arafat.

No comments: