SOKO LA MABIBO CORONA BASI, LANUFAIKA, KUTENGEENEZEWA VIZIMBA VYA KUNAWIA MIKONO KWA KILA MTUMIAJI.

Taasisi isiyo ya kiserekali ya Vijana Think Tank (VTT)  @vijanathinktank ambayo inajumuisha vijana zaidi ya 250, ambayo ilianza kama jukwaa kupitia group la WhatsApp, siku ya leo wamekabidhi vizimba vitatu vya maji kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo baada ya kuchangishana pesa kupitia kundi hilo la WhatsApp na kuamua kupamabana na janga la Corona kwa kuelekeza nguvu zao kwenye masoko mkoani Dar Es Salaam.

Akiongea mwakilishi wa taasisi ya Vijana Think Tank (VTT)  @vijanathinktank Bi. Lilian Madeje amesema kuwa waliamua kuchangishana pesa kupitia jukwaa hilo la WhatsApp ili kusaidia jamii badala ya kujadiliana mambo yao binafsi kama baadhi ya majukwaa mengine ya WhatsApp yanavyofanya.

Ameongeza kuwa waliamua kuungana na NVRA ambao pia ndio waliolewa ridhaa ya kuwakilisha kusimamia ujenzi wa mradi huu, kuanzia kujengwa mpaka leo umekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo.

Akiongea Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mh. Beatrice Dominic, amewapongeza vijana hao wa Kitanzania ambao waliona na kuamua kujitoa kwa kuona umuhimu wa kupambana na janga hili kwa kuchangishana pesa kupitia Group la WhatsApp, mitandao ya kijamii na hata ana kwa ana.

Mradi huo ambao umekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo umegharimu kiasi cha Tsh milioni 3.7 hadi kukamilika ukiwa na vizimba vitatu vya kunawia mikono kwa kila mtu atakayeingia sokono.

Kwa sasa wameanza na soko la Mabibo na baadae wataenda katika masoko mengine yaliyopo jijini Dar Es Salaam yakiwemo Kariakoo, Shekilango, Sinza na mengine.




No comments: