CWT YAAHIDI KUFANYA MAPINDUZI KATIKA SOKA HAPA NCHINI-ALAWI

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimeahidi kufanya mapinduzi katika soka, kwa kuwa na timu imara itayoshiriki Ligi za ndani na nje ya nchi.

Hatua hiyo inatokana na mikakati kabambe inayotarajia kuwekwa na Walimu kupitia uongozi wa Makao Mkuu, mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa chama hicho unaotarajia kufanyika Mei 28 mwaka huu.

Hayo yalielezwa na Mwalimu Abubakari Alawi akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Kibaha,ambaye ni mgombea wa nafasi ya Mhazi kwenye uchaguzi huo ndani ya chama hicho, alipojibu swali kuhusiana na mikakati ndani ya soka.

Alawi ambaye ni Katibu wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani COREFA, aliyasema hayo akizungumza na Waandishi wa habari mjini Kibaha ambapo alibainisha ,Walimu wamedhamiria kuikomboa nchi kwenye medani hiyo hususani michuano ya Kimataifa.

"Nakumbuka Rais wetu dkt.John Magufuli alishawahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa ana hamu ya kuiona timu itayoipeperusha nchi kwenye michuano ya Kimataifa kwa mafanikio, tunasema kuwa Walimu tutakata kiu hiyo ya wa-Tanzania," alisema Alawi.

Alawi ambaye ni mgombea wa nafasi ya Mhazini ndani ya chama hicho cha Walimu Taifa akitetea nafasi hiyo, aliongeza kuwa tayari wameshaweka mikakati madhubuti itayokwenda kutekelezwa baada ya uchaguzi huo.

Alieleza, vilabu vingi vinavyoshiriki ligi mbalimbali zina wachezaji ambao ni walimu.

Aliongeza kwamba kwa sasa kuna baadhi ya wilaya zina timu na kushiriki Ligi ngazi zilizopo, lakini moja ya mikakati iliyopo ni kwamba baada ya kufanyika kwa uchaguzi watakaa kuhakikisha hilo wanaliwekea mikakati madhubuti.

No comments: