RC PWANI ATOA SIKU SABA UONGOZI WA HALMASHAURI YA BAGAMOYO KUKAMILISHA HOJA 38 ZA CAG
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza wakati wa kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kilichoandaliwa kwa ajili ya kujadili majibu ya hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisoma kwa umakini ripoti ya hoja mbali mbali ambazo zimeandikwa katika kitabu maalumu na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali wakati wa kikao hicho cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Ally Ally akifungua kikao rasmi wakati wa mkutano maalumu wa baraza la madiwani ambao uliandaliwa kwa ajili ya kupokea na kujadili majibu ya hoja za mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2018 /2019.
mkaguzi wa Ofisi ya Taifa ya ukaguzi na udhibiti wa hesabu za serikali (CAG) wa Mkoa wa Pwani Mwajuma Kwipunda akisoma taarifa katika mkutano huo maaalumu wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakiwa wameketi katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kupokea taarifa na kujadili majibu ya hoja kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu wa serikali.
Mkuu wa Wilaya ya Bgamoyo Zainabu Kawawa akiwa anazungumza jambo katika mkutano huo maalumu wa baraza la madiwani kwa ajili ya kupokea na kujadili mambo mbali mbali ikiwemo hoja ambazo zimetolewa na mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali
Baadhi ya wakuu wa idara wakiwa wanafuatilia mkutano maaalumu wa baraza la madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo amabo ulianaliwa kwa ajili ya kupokea na kujadili majibu ya hoja kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali kwa mwaka wa 2018/2019.(picha na Victor Masangu)
…………………………………………………………………………………………….
VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amechukizwa na kuona miradi ya maendeleo ipatayo 42 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 1 katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo haijakamilika kwa wakati hadi sasa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya watumishi na watendaji kufanya kazi kwa mazoea na uzembe hali ambayo inasababisha hasara kubwa na kukwamisha juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi maendeleo hivyo wote watakaobainika kuhusika na ubadhilifu wowote wa fedha wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa mkutano maaalumu wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wenye lengo la kupokea na kujadili majibu ya hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) kwa kipindi cha mwaka wa hesabu kwa mwaka wa 2018/2019.ambapo pia ametoa muda wa siku saba kwa uongozi wa halmashauri hiyo kufunga hoja zote 38 ambazo bado hazijakamilika hadi sasa kwani ili kuendana na maagizo yaliyotolewa na serikali ya Mkoa.
Ndikilo alisema kwamba katika taarifa amabayo imetolewa na mdhibiti na wa hesabu za erikali CAG imeweza kueleza kuwa kuna baadhi ya miradi ambayo bado ijakamilika wakati fedha zake zimeshatolewa hivyo kuna dalili za baadhi ya watendaji kutowajibika kikamilifu katika uetekelezaji wa majukumu yao.
“Fedha zimetolewa kabisa shilingi bilioni 1 na milioni 24 lakini mimi nashangaa miradi 42 bado haijakamilika kwa wakati kabisa hii kwa weli sio sahihi hata kidogo hapa inatakiwa ndugu zangu madiwani wa baraza hili kuangalia kwa makini maana hii miradi ni mingi kwa hiyo mimi ninachokiomba miradi hii iweze kukamilika kabisa kwa wakati na kwa wale watumishi ambao watakuwa wamehusika katika uzembe huu ni lazima wachukuliwa hatua kali z akisheria.
Aidha Mkuu huyo aliongezea kuwa kwa sasa inatakiwa hoja zote ambazo ziliitajika kukamilishwa kwa kipindi hiki ni lazima zifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo maana ni agizo ambalo lilishatolewa na serikali ya Mkoa kwa hiyo mimi naagiza ndani ya siku saba kwa maana ya wiki moja hoja hizi 38 na kipindi cha mwak 2018/2019 ni lazima zikamilika pamoja na zile hoja nyingine za miaka iliyopita.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amesema licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi kwa mfululizo kuanzia kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 1019 lakini watendaji na watumishi wanapaswa kubadilika kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi hasa katika suala zima la kudhibiti mianya ya upotefu wa mapato pamoja na kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa katika miradi ya maendeleo.
Kawawa alibainisha kwamba katika halmashauri ya Wilaya ya Bgamoyo kumekuwepo na changamoto mbali mbali katika suala zima la ukusanyaji wa mapato hivyo kunahitajika juhudi z amakusudi katika kuhakikisha mashine ambazo zinatumika katika ukusanyaji wa mapato hayo zinakuwa zinawashwa kwa lengo la kuweza kuongeza makusanyo tofauti na ilivyokuwa kwa sasa.
“Hii hali ya ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ya Wilaya ya Bgamoyo sio mzuri ndio ni kweli tumefnikiwa kupata hati safi kwa awamu nne mfululizo lakini sisi kama viongozi ni lazima tufuatilie kwa umakini kuhusiana na ukusanyaji w amapato haya mbali mbali maana nasikia kuna mashine nyingine zinakuwa zimeimwa kwa kipindi cha muda mrefu sasa hii ni hatari sana lazima mapato yetu yapotee tuu kutokana na uzembe wa baadhi ya watu,”alisema Kawawa.
Naye mkaguzi wa Ofisi ya Taifa ya ukaguzi na udhibiti wa hesabu za serikali (CAG) wa Mkoa wa Pwani Mwajuma Kwipunda alibainisha kwamba halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 licha ya kuwepo kwa mapungufu ya kutokamilisha mapendekezo kwa wakati imefanikiwa kupata hati safi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa halmashauri hiyo amefarijika kupokea hati safi kwa mara ya nne mfululizo na kuahidi kuyafanyia kaiz kwa vitendo maagizo yote nane ambayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa kuhusina na mambo mbali mbali katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maeneleo pamoja na utekelezaji wa hoja ambazo bado hazijafanyiwa kazi.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo iliyopo Mkoa wa Pwani licha ya kupatiwa hati safi mfululuzo kuanzia kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019 kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) lakini bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika masuala ya ukusanyaji wa mapato pamoja na kutokamilisha kwa baadhi ya miradi ya maendeleo kwa wakati.
No comments: