RAIS MAGUFULI:WATANZANIA OONDOENI HOFU KUHUSU CORONA, ENDELEENI KUCHAPA KAZI


*Awahakikishia watumishi wote wa umma kuendelea kulipwa mishahara yao

RAIS Dk.John Magufuli tangu tanga la Coroa limeibuka kila nchi inao utaratibu wake wa kushughulika na tatizo hilo na kwa Watanzania hakuna sababu ya kuwa na hofu yoyote na waendelee kuchapa kazi.

Ametumia nafasi hiyo kuwahakikisha watumishi wote wa umma wakiwemo walimu ambao ndio wengi zaidi kuwa Serikali itaendelea kuwalipa mshahara hadi shule zitakapofunguliwa ingawa kuna nchi nyingine zimeshindwa kulipa mishahara watumishi wake.

Akizungmza leo Mei 3 mwaka 2020 wakati akimuapisha Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Mwigulu Nchemba huko Chato mkoani Geita Rais Magufuli amefafanua hatua kwa hatua namna ambavyo Serikali imeendelea kushughulikia janga la Corona na hali ilivyo.

Hata hivyo, amesema uzoefu unaonesha kila linapotoea gonjwa jipya watu hupata hofu na wasiwasi, wakati wa Ukimwi unaingia nchini kupitia Mkoa wa Kagera kwa mara ya kwanza watu waliogopa sana, hata waliokuwa hawana Ukimwi nao walipakaziwa kuwa na Ukimwi.

"Leo hii ukizungumza kuna mtu ana Ukimwi bado watu wengine wanakwenda kuposa na kuoa na maisha yanaendelea kwasababu hofu yaugonjwa huo imeondoka.Kwa hiyo kwenye magonjwa watu wa umri wangu wanakumbuka, siku za nyuma wakati ugonjwa wa surua umeingia "Ilikuwa ukisikia kuna familia kuna surua hata kwenda kusalimia unaogopa kwamba mtaambukizwa surua lakini leo ni ugonjwa wa kawaida na hofu imeondoka,"amesema Rais Magufuli.

Amefafanua ndivyo hivyo hivyo na kwa magonjwa mengine ambayo yamekuwa yakitokea nchini.Magonjwa kama TB, magonjwa kama Ukoma yalikuwa yanatisha na kutia hofu."Ukimuona mtu mwenye ukoma unajiliza kuhusu maisha yake yatakuaje lakini sas hakuna tena hofu kwenye magonjwa hayo."

Pia amesema yametokea magonjwa megi kama Zika na Ebola katika nchi nyingine mbalimbali na hofu zilijengeka ."Niwaombe Watanzania tuondoe hofu na kubwa zaidi tuendelee kuchukua tahadhari.

"Tusihusishe hili la Corona kwenye kwenye uchumi wa nchi yetu, mimi nimepata uzoefu katika miezi miwili au mitatu tangu ugonjwa huu uingie.Nchi yetu asilimia 49 ya watumishi ni walimu ambao ndio wengi zaidi kuliko wengine.

"Lakini tumeendelea kulipa mishahara bila hata wao kufundisha, kuna nchi zimeshindwa kulipa mishahara.Nataka kuwathibitisha walimu tutaendelea kulipa mishahara yenu hadi shule zitakapofunguliwa, pia watumishi wengine wote tutaendelea kuwalipa mishahara na hii ndio dhana ya kutokuumiza uchumi kwa tatizo hili ambalo litaondoka,"amesema Rais Magufuli.

No comments: