Mitaa ya Nairobi na Mombasa yawekewa amri ya kutotoka nje saa 24
Wakaazi wa Maeneo ya Eastleigh jijini Nairobi na Old towm mjini Mombasa nchini Kenya hawatoruhusiwa kutoka katika maeneo hayo katika kipindi cha wiki mbili zijazo kuanzia saa moja usiku wa Jumatano Mei 6, 2020.
Hatua hiyo inalenga kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona katika maeneo mengine ya miji ya Nairobi na Mombasa huku wagonjwa wengine wapya 47 wakitangazwa na kufanya idadi ya maambukizi kufikia watu 580.
Akizungumza na vyombo vya habari Waziri wa Afya Mutahi kagwe amesema kwamba kati ya wagonjwa hao 47, 32 wanatoka Mombasa huku 11 wakitoka Nairobi.
Amesema mtaa wa Bondeni ambao wakaazi wake wamekuwa wakiuka masharti ya afya yaliotolew na serikali una wagonjwa 18 wapya huku mtaa wa Estleigh ukiripoti wagonjwa 5 wapya.
Waziri Kagwe ameoonya mitaa mingine kwamba itachukuliwa hatua kama hiyo iwapo itaendelea kukiuka maagizo ya Kiafya na kusababisha maambukizi ya kiwango cha juu.
Waziri huyo pia ameagiza kwamba mikahawa iliopo katika maeneo hayo iendelee kufungwa wakati wa amri hiyo ya kutotoka nje.

No comments: