MBUNIFU WA NYWELE ANAYEISHI NDANI YA NDEGE


Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

JO Ann mbunifu wa nywele amebadilisha ndege iliyotelekezwa katika moja ya karakana huko Greenwood kwa kutengeneza vyumba vitatu, sehemu ya kupumzika na jiko.

Ann aliibadilisha ndege hiyo ya abiria Boeing 727  na kuiita jina la Rais wa Marekani Donald Trump.

Makazi hayo yanapatikana huko Benoit, Mississippi karibu na uwanja wa ndege wa Greenwood.

 Imeelezwa kuwa Ann alianzisha makazi hayo mapya aliyoyaita "Nyumba bora ulimwenguni"  mara baada ya makazi yake kukumbwa na dhoruba ya barafu.

Ndege hiyo yenye urefu wa mita 42 ilianza kufanya kazi kuanzia Mei 1968 hadi Septemba 1993 huku ikielezwa kuea iligharimu dola 2000 kuinunua na inakadiriwa marekebisho yake yatagharimu zaidi dola 30,000.



 

No comments: