KUNRADHI NDUGU SIA LYIMO
Mnamo tarehe 30/04/2020 tulichapisha habari kuhusu sakata la wafanyakazi wa Impala Group na Hoteli ya Naura iliyopo Arusha ambapo mwakilishi wetu huko alileta habari kwamba alimhoji Ndugu Siya Lyimo, jambo ambalo imeonekana siyo kweli na kuleta usumbufu kwa Ndugu Sia Lyimo na kuhatarisha kumchonganisha na viongozi wa mkoa na wilaya ya Arusha.
Tunaomba radhi kwa ndugu Sia Lyimo kwa taarifa hiyo ambayo tunakukiri kwamba inaonesha hakuwahi kuhojiwa na mwakilishi wetu huyo; na ambaye kwa kosa hilo tunamchukulia hatua kali kwani ni kinyume cha maadili ya taaluma na weledi wa tasnia ya habari na pia kwa Blog inayoheshimika kama hii.
UONGOZI
MICHUZI BLOG
No comments: