JAFO AITAKA TUME YA UTUMISHI WA WALIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIMU NCHINI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Selemani Jafo ameutaka uongozi mpya wa Tume ya Utumishi wa Walimu kutatua changamoto za walimu ili kuwatia moyo katika kutimiza majukumu yao.

Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati wa kuapishwa wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu .

Jafo amesema kuwa Tume hiyo ndani ya wiki moja ikafanyie kazi mashauri ya rufaa 110 ili walimu waweze kutekeleza majukumu yao katika ubora unaohitajika.

Akizungumza amesema kuwa Tume inatakiwa kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu hasa katika kushughulikia uboreshaji wa upandaji wa madaraja ya walimu.

“Nendeni mkawe sikio la walimu na kusimamia nidhamu ya walimu ili kuleta utendaji bora katika kutekeleza majukumu yao”, amesema Jafo.

Amesema kuwa tume hiyo inatakiwa kufanya kazi katika ubora unaohitajika ili kuleta uwajibikaji katika shughuli za walimu hapa nchini

Waziri Jafo ametoa wito kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Prof. Willy Lazaro Komba kutoa ushirikiano kwa wajumbe wake ili kuweza kufanyikisha shughuli za utendaji katika ubora unaohitajika na walimu wanao wahudumia.

PiJafo amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa maono yake juu ya kupambana na janga la Corona kwa kutozuia shughuli za watanzania ila kuwataka kuchukua taadhali na wananchi kuendelea na uzalishaji wao katika kutafuata kipato chao.

Kwa kuongezea Jafo ametoa rai kwa watanzania kujifukizia (kupiga nyungu) kwa awamu ya pili ili kuimarisha afya zao zaidi na kupambana na kupambana na corana kwani vita hii haichagui silaha..

Naye Mwenyekiti wa Tume hiyo Prof. Willy Lazaro Komba akitoa neno la shukurani amesema kuwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo ili wanao wahudumia kupata huduma bora wanazotarajia kutoka kwao.

“Tuko tayali kuanza kazi ili kuwatumikia tunao waongoza na kufanyikisha ubora katika shughuli zao” ameeleza Prof. Komba.

Prof. Komba ametoa wito kwa wajumbe kutoa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMIESMI) Selemani Jafo akimkabidhi vitendea kazi mmoja wa wajumbe wapya waliyoapishwa wa Tume ya Utumishi wa Walimu  leo Jijini Dodoma baada ya kuapishwa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMIESMI) Selemani Jafo akizungumza na uongozi mpya wa Tume ya Utumishi wa Walimu leo wakati wa kuwaapisha wajumbe wa Tume hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMIESMI), Selemani Jafo akimuapisha Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Prof. Willy Lazaro Komba leo Jijini Dodoma.
 

No comments: