DK.MAGUFULI AWASHANGAA VIONGOZI WA DINI WANAOZUIA WAUMINI WAO KWENDA NYUMBA ZA IBADA, AWATAKA KUSIMAMA KATIKA VIAPO VYAO
Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
RAIS Dk.John Magufuli amesema kutokana na uwepo wa ugonjwa Covid-19 kuna baadhi ya viongozi wa dini wamemsahau Mungu ambaye wamekuwa wakituhubiria waumini wao kwa siku zote.
Akizungumza leo Mei 3 mwaka 2020, Rais Magufuli amesema kuwa inashangaza unapoona viongozi wa dini wanamsahau Mungu kwasababu tu ya uwepo wa Corona."Licha ya kuapa kwa dini zao, wamemuacha Mungu na kwenda kubaki kujali ubinadamu.Ndio wamekuwa wakihamasisha kuwaambia wamumini acheni kwenda kwenye nyumba za ibada.
"Hiki ndio kipindi cha kuwapima viongozi wa dini. Unapozuia watu kwenda kwenye nyumba za ibada, ni mambo ya ajabu.Wakati mwingine hilo Kanisa au Msikiti hukujega wewe, ache waumini wengine waendelee, kama wewe kiongozi wa dini unaogopa acha wengine waende wakumuabudu Mungu wao,"amesema Rais Magufuli.
Amesema kwenye vitabu vya dini vinaeleza majaribu ambayo yaliwatokea watu wa Mungu lakini walishinda majaribu hayo na kuyavuka salama, hivyo hata Tanzania nako ni wajibu wa kila mtu kusimama na imani yake na si kuendelea kutishwa na kuzuiliwa kwenda kufanya ibada.
Rais Magufuli ameongeza kuwa kuna wakati shetani hutumia viongozi wa dini kufanikisha mambo yake, na huenda kwenye hili shetani kuna baadhi ya viongozi wa dini anawatumia."Watanzania tumtangulize Mungu kwenye hili, tutavuka salama, Mungu yuko pamoja na sisi, tuendelee kumtumainia yeye kwa kila jambo."
No comments: