BHARAT JAIN, OMBAOMBA ALIYEVUNJA REKODI KWA UTAJIRI DUNIANI

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
NI kiasi gani cha fedha unatengeneza kwa mwaka? au mwezi? inaweza kuwa ni mamilioni ya fedha ila inashangaza kuona watu wanaoomba fedha barabarani wanatengeneza fedha kukuzidi, na inafikirisha sana juu ya nguvu waitumiayo ombaomba kuzunguka barabarani hadi kuufikia utajiri na kuvunja rekodi.

Bharat Jain (53) raia wa India anaelezwa kuwa ndiye ombaomba tajiri zaidi aliyewahi kutokea ulimwenguni, Jain anatokea Mumbai na shughuli zake za kuomba msaada huzifanya katika maeneo ya Azad Maidan na Shivaj Terminus.

Jain hupata Rupia 2000 hadi 2500 kwa siku akiomba kwa masaa nane hadi kumi na kwa mwezi huingiza rupia 75000 sawa na dola za kimarekani 1000.

Kupitia kazi hiyo Jain alifurahia maisha na aliweza kumiliki nyumba 2 za biashara huko Patel Nagar, duka lililopo Bhandup pamoja na kioski kilichouza sharubati na katika nyumba alizopangaisha alilipwa si chini ya Rupia 10000.

Mwaka 2015 baada ya kifo chache kilichotokana na ajali ya treni polisi waligundua kuwa Bharat Jain kupitia kuomba barabarani aliingiza Rupia70000 hadi 80000 kwa mwezi na hiyo ni kupitia nyaraka walizozikuta kwenye makazi yake.

Pia iligundulika alikua na salio la kutosha pamoja lundo la shilingi zipatazo sandarusi moja ambazo zilizokutwa katika makazi yake huko Burju.

Jain aliishi mwenyewe hata majirani zake hawakufahamu kumhusu ni nyaraka pekee zilizomtambulisha huku kijana wake akiorodheshwa kama mrithi.

Mwaka huo huo ombaomba mwingine Krishna Kumar Gite aliteka vyombo vya habari kwa kukusanya Rupia 40000 hadi 50000 kwa mwezi pamoja na kumiliki nyumba huko Nala Sopara, Mumbai.

No comments: