TAAnet YAISHAURI SERIKALI BAR NA VILABU VYA POMBE KUFUNGWA WAKATI HUU WA MAPAMBANO NA MARADHI YA COVID-19
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mtandao wa Wadau wanaopambana na unywaji pombe kupita kiasi–TAAnet wameishauri serikali kutoa tamko la kufunga bar na klabu zote za pombe ili kudhibiti unywaji wa pombe na kuleta madhara makubwa kwa
binadamu ikiwemo kushusha kinga za mwili.
Hayo yamesemwa na mtandao huo wa TAAnet wakiungana kwa pamoja na serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya korona na kutambuliwa kama covid-19.
Katibu wa TAAnet Gladness Munuo amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa umma juu ya madhara ya unywaji pombe kupita kiasi ambapo Jamii imekuwa ikisumbuka na magonjwa mbalimbali yanayoletwa na matumizi ya pombe kupita kiasi kama vile maradhi ya moyo, ini, saratani n.k.
Amesema,hali kadhalika katika mapambano dhidi ya janga la gonjwa la covid-19 hawana budi kuweka mkazo kwa kuiomba serikali ya
Tanzania kuangalia upya utengenezaji, usambazaji na unywaji wa pombe nchini kwa wananchi wake ikiwa ni moja wapo ya kujikinga na maambukizi ya ungonjwa wa homa ya mapafu (covid-19).
"Taarifa pamoja na tafiti mbali mbali zimeshaeleza kuwa, mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini awe kijana au mzee ni rahisi kupatwa na virusi vya korona vinavyoleta ungonjwa wa covid-19 kwa maana ya kupata homa kali ya mafua, kwa kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi moja wapo ya madhara makubwa kwa binadamu ni kushusha kinga za mwili ambapo athari yeyote ya magonjwa ikiwepo huu wa covid-19 huweza kumpata mtu wa aina hiyo na kuleta maafa makubwa," amesema.
Munuo amesema, TAAnet ikiwa ni muungano wa mashirika zaidi ya 20 yanayopinga matumizi mabaya ya pombe nchini, kwa pamoja wanaiomba Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto kutambua na kubainisha
aina za pombe ambazo katika kipindi hiki cha maradhi yanayoambukizwa na virusi vya korona kusitishwa kabisa kutengezwa na kusambazwa nchini ikiwa ni hatua ya kuunga mkono serikali yetu katika kukabiliana na gonjwa la covid-19.
"Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopambana na kudhibiti unywaji pombe kupita kiasi nchini Tanzania, kwa ujumla tuna sababu ya kuhakikisha Wa Tanzania wote mijini na vjijini, Wazee kwa vijana wanakuwa salama ki Afya, Kiuchumi na hata katika maendeleo yao kimazingira n.k. Hivyo basi, tunatoa RAI kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa katika kipindi hiki cha mapambano na ugonjwa wa covid-19 vilabu vya pombe, bar na ‘pub’ zinazojihusisha na biashara za pombe nchini kufungwa au kuwekewa utaratibu mpya mara moja.
Katika kuhakikisha kuwa wa Tanzania wanakuwa salama,"
Aidha, ametolea mfano kwa baadhi ya nchi za Afrika zilizozuia uuzwaji wa Pombe katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya kukabiliana na gonjwa la Covid -19.
"Zipo baadhi ya nchi zimechukua hatua kuhakikisha kuwa matumizi ya pombe zote yanadhibitiwa, nchi kama Zimbabwe, South Africa, Zambia na nchi nyingine kama Uganda zimepiga marufuku uendeshaji wa vilabu vya pombe na Kenya wako katika harakati za kupinga usambazaji
wa bidhaa ya pombe.,"
Katika hali kama hii Tanzania haiko katika kisiwa, na kutokana na mipaka kuwa wazi inasemekana kuwa baadhi ya walevi huvuka mipaka kuja Tanzania kunywa pombe. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO- Septemba,2018), Watu zaidi ya milioni 3 hufariki duniani kote kutokana na matumizi mabaya ya pombe. Zaidi ya robo tatu (3/4) ya vifo hivi vilikuwa ni vya wanaume. Kwa ujumla, matumizi mabaya ya pombe husababisha zaidi ya asilimia 5 ya mzigo wa magonjwa duniani. Taarifa kama hii pia inapatikana katika Taarifa ya hali ya Dunia kuhusu unywaji pombe na afya 2018(Global status report on alcohol and health 2018).
Matumizi ya pombe na athari zake ni tatizo linalozidi kukua nchini Tanzania, na linapaswakudhibitiwa kwa haraka iwezekanavyo hasa katika wakati huu Taifa letu na mataifa mengine duniani yako katika mapambano na ugonjwa unaoletwa na virusi vya korona.
Aidha, tafiti zimeonyesha kuwa wanaotumia pombe za kienyeji ambao kwa takwimu Tanzania Jamii ni wengi, wao huathirika zaidi kwa ajili ya mazingira ya utengenezaji na hata unywaji. Kutokana na athari za covid-19 TAAnet inazikumbusha taasisi husikapamoja na Serikali kuangalia kwa haraka namna ya kudhibiti UTENGENEZAJI, USAMBAZAJI NA UNYWAJI WA POMBE katika kipindi hiki cha mapambano na covid-19ili kunusuru maisha ya vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa pamoja na wazee
yanayoendelea kuharibika kila siku.

No comments: