MTANZANIA ATOA USHUHUDA HALI ILIVYO NCHINI ITALIA BAADA YA MLIPUKO WA VIRUSI VYA COVID-19 ‘WAPO LOCKDOWN’
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Hali ya Maambukizi ya Virusi vya COVID-19 imetajwa kuwa si shwari nchini Italia kwa Wananchi wengi nchini humo kujifungia ndani (Lockdown) kutokana na kasi ya maambukizi ya virusi hivyo vilivyosambaa sehemu nyingi duniani kwa sasa.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Parma (Parma Unniversity) kilichopo nchini Italia, Mtanzania Frank Charles amezungumza na Michuzi Blog, Michuzi TV ameeleza hali si shwari nchini humo kutokana na Wananchi wengi kujifungia ndani muda wote kuogopa Maambukizi ya Virusi hivyo.
Frank ameeleza kipindi cha Sikukuu za Pasaka, Wananchi hao wengi wamesheherekea sikukuu hiyo wakiwa majumbani wakihofia maambukizi. Amesema kuna udhibiti mkubwa wa Askari wa nchi hiyo kusambaa sehemu mbalimbali kuzuia mikusanyiko ya watu.
“Hata kama kuna Mgonjwa nyumbani kwako kuna namba zimewekwa ili upige na wahudumu wa masuala ya afya waje kufanya matibabu, Wagonjwa kwenye vituo vya afya ni wengi kuliko Madaktari na Vifaa Tiba, ndio maana wameweka namna ya kufanya matibabu nyumbani,” amesema Frank.
Amesema Wanafunzi wa Tanzania wapo katika hali shwari, isipokuwa changamoto ni kufungwa maduka mengi, hivyo kufanya foleni katika sehemu za Maduka ya Vyakula na Dawa za Matibabu ya kawaida. Ameeleza Serikali ya nchi hiyo imejitahidi kuwafadhili baadhi ya Wanafunzi kujikimu Kiuchumi katika kipindi hiki.
“Chuo chetu cha Parma kimeweka namna ya kusoma kupitia Mitandao ‘Online’ ili kuzuia kutoka nje, kiukweli kuna baadhi ya vitu vinakuwa vigumu kusoma kupitia mtandao, kutokana na kufanya kitu Mtandaoni sio sawa na kama upo Chuoni, lakini hakuna jinsi tunasoma hivyo hivyo,” ameeleza Frank.
Kwa upande mwingine, Frank ameeleza kuwa tayari wameonana na Ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo Mjini Rome, mwanzoni tu baada ya virusi hivyo kusambaa, “Tayari tumeujulisha Ubalozi wetu wa Tanzania kuwa sisi tupo Chuo Kikuu cha Parma, wanajua kuna Watanzania huku”, amesema
Frank amewaasa Watanzania kuzingatia maagizo yanayotolewa na Mamlaka husika ili kukabiliana na Maambukizi ya Virusi hivyo vya COVID-19 vinavyoisumbua Dunia na kuchukua tahadhari mapema, amesema endapo kama watafuata maagizo hayo itasaidia sana kupunguza Maambukizi hayo yanasumbua dunia kwa sasa.

Baadhi ya Miji iliyopo nchini Italia, muonekano katika Kipindi hiki cha Mlipuko wa Maambukizi ya Virusi vya COVID-19.
No comments: