KIGOGO BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA AMBAYE NI RAIA WA NIGERIA ANASWA JIJINI DAR, WAMO PIA WATANZANIA WAWILI...



Watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya wakiwa chini ya ulinzi baada ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kuwanasa jijini Dar es Salaam.
Tanki la maji machafu ambalo lilitengenezwa na watuhumiwa hao wa biashara ya dawa za kulevya kwa ajili ya kuwekea dawa hizo kama sehemu ya kuzificha.Hata hivyo tanki hilo walichelewa kulikamisha na hivyo dawa hizo kuzihifadhi ndani ya nyumba.
 

Na Ripota Wetu,Michuzi TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya jana tarehe 15 April 2020, imefanikiwa kumkamata kigogo wa dawa za kulevya raia wa Nigeria Kanayo David  Chukwu (39) mkazi wa Masaki jijini Far we Salaam.

Pia inawashikilia raia wawili wa Tanzania Alistair Amon Mbele(38) ambaye ni mkutubi wa Chuo Kikuu cha Aghakan jijini Dar es Salaam, mkazi wa Mbezi Kibanda cha mkaa na Isso Romward Lupembe (49) ambaye Ni mkazi wa Mbezi Louis na Changanyikeni jijini.

Watuhumiwa wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin zinazokadiliwa kuwa na zaidi ya kilogramu 270 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye moja ya nyumba iliyopo Mbezi kibanda cha mkaa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,  Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa muda mrefu  nchini na kwamba  Mamlaka imefanikiwa kukamatwa kutokana na jitihada ushirikiano uliopo kati ya nchi yetu na nchi  nyingine katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya duniani kutokana na utaratibu wa kubadirishana taarifa ambazo husaidia kurahisha ukamataji huo.

“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyombo mbalimbali vya usalama ndani na nje ya nchi tulianza kuwafuatilia toka tarehe nane na kufanikiwa kuwaweka mtegoni tangu wakiwa wanateremsha mzigo na kufanikiwa kuwakamata.

"Pia watuhumiwa hao walikuwa wamefanya maandalizi ya kupokea mzigo huo kwa kujenga tenki la maji machafu ambalo liliwekwa chemba juu ya kuhifadhia dawa hizo  na bahati mbaya mzigio uliwahi kufika kabla tenki halijakamilika, hivyo kulazimika kuzihhifadhi ndani ya nyumba,"amesema
Kamishna Kaji.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania kwa  kutoa taarifa pale wanapoona matukio yasiyo ya kawaida kwa usalama.

 “Kilo hizi ni nyingi sana zingeingia mtaani zingeathiri nguvu kazi ya vijana wetu huko mitaani kwa kiasi kikubwa. Ninasikitika kuona bado kuna watu wasio na utu wanaendelea kujitafutia kipato kwa njia hii haramu bila kujali. Ninatoa rai kwa watanzania walio tayari kuwapambania watoto wao kuendelea kushirikiana na Mamlaka kuwafichua watu hawa bila woga," amefafanua.

Ameongeza kuwa watuhumiwa wako mikononi mwa Mamlaka na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika ili sheria ichukue mkondo wake.

No comments: