VIDEO: Azam Yapita Kwa Kishindo, Yaipiga Kenema Bao 3-2
KILA mtu ashinde kwake! Azam imekataa uteja kwa mara ya pili baada ya kuwachapa Fasil Kenema kwa mabao 3-2 kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam wanaonolewa na kocha Ettiene Ndayiragije jana Jumamosi walitumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex baada ya kuwazima Kenema na kusonga mbele kwenye hatua ya kwanza ya kombe hilo.
Muivory Coast, Richard Djodi aliifungia Azam mabao mawili na la ushindi likitupigwa na Obrey Chirwa.
Djodi alikua mwiba kwa Kenema ambao walikuwa na kazi kubwa ya kumzuia kutokana na mzuka na kiwango alichokuwa nacho.
Azam FC iliyofungwa 1-0 ugenini, licha ya kupata mabao hayo walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda mabao mengi zaidi kwenye mechi hiyo lakini kipa wa Kenema alipambana kuokoa misala iliyokuwa ikimuandama.
Wachezaji wa Kenema kadri muda ambavyo ulikua ukienda walitepeta kutokana na uwezo wa Azam waliokuwa wakiuonesha katika dakika za mwisho.
Baada ya mechi kumalizika Kenema ambao walikaa moja ya hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikwea pipa na kurejea kwao Ethiopia.
MAGOLI YA AZAM FC VS FASIL KENEMA 3 -1
The post VIDEO: Azam Yapita Kwa Kishindo, Yaipiga Kenema Bao 3-2 appeared first on Global Publishers.
No comments: