Mapambano ya Ubingwa wa Afrika Mashariki na kati Yafanyika Jijini Dar
Mapambano ya Ubingwa wa Afrika Mashariki na kati, yamefanyika kwa kishindo usiku wa kuamkia leo Agosti 24, 2019 Club 361 Mwenge jijini Dar es Salaam . Mgeni rasmi Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Jeshini, Meja Jenerali Alfred Kapinga
Mabondia wametifuana kuwania ubingwa wa Afrika Mshariki huku wajeda nao wakijiwinda na michuano ngumi za ridhaa ya kimataifa ya majeshi yanayotarajiwa kufanyika mapema hivi karibuni.
Katika mtifuani huo mkanda wa Ubingwa Afrika Mashariki uzito wa Unyoya ulianza kupiganiwa na Issa Nampepechena Nassibu Ramadhani pambano lililokuwa na raundi kumi ambapo Nassibu aliibuka na ushindi.
Pambano lingine la Ubingwa wa Afrika Mashariki uzito wa Bantam nalo lilikuwa la raundi kumi kati ya bondia, Tonny Rashid na Haidari Mchanjo ambapo Tonny ndiye aliyeutwaa mkanda huo.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL
The post Mapambano ya Ubingwa wa Afrika Mashariki na kati Yafanyika Jijini Dar appeared first on Global Publishers.
No comments: