Kocha Akivaa Hovyo Uwanjani, Kutimuliwa

 

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera

BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPBL) imesema imebadilisha baadhi ya mfumo wa uendeshaji wa masuala mbalimbali ikiwemo suala la mavazi ya makocha. Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kuwa mabadiliko hayo yanaendana na mpango wa kuboresha ligi.

 

“Masuala tuliyoyaangalia zaidi ni kuhusu suala zima la wachezaji wa kigeni hawatapewa leseni za kucheza hadi wapatiwe vibali vya makazi na kazi, pia wachezaji wote wa kigeni watakaosajiliwa msimu ujao lazima wawe wanacheza timu za taifa au ligi kuu nchini mwao.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems.

“Klabu zote za ligi kuu zinatakiwa zisajili wachezaji watatu wa kutoka U-20 na wapatiwe nafasi ya kucheza. “Timu za ligi kuu zitapungua kutoka 20 za sasa hadi 16 katika msimu miwili ijayo, tunaanza kupunguza timu mbili msimu ujao kisha mbili nyingine katika misimu inayofuata lakini michezo ya Play Off itakuwa vilevile, pia tunahitaji Ligi Daraja la Kwanza na la pili ichezwe kwa ligi moja na si ya makundi kama ilivyo sasa.

 

“Pia katika mabadiliko hayo, timu mwenyeji ndiye atakayetakiwa kuandaa gari la wagonjwa katika mchezo husika pamoja na waokota mipira na iwapo timu mwenyeji haitafanya hivyo itapokonywa pointi na makatibu wake kupewa adhabu.

 

“Tumefanya hivi kwa kuwa timu mwenyeji anachukua asilimia 60 ya mapato, vilevile kamisha wa mechi anatakiwa ajue mapema vazi la benchi la ufundi katika pre-match meeting na kama kocha atavaa tofauti ijulikane mapema na avae vizuri na akivaa tofauti kamishna ataruhusiwa kumuondoa.

 

“Upande wa makocha wa ligi kuu wanatakiwa wawe na leseni B ya Caf na Ligi Daraja la Kwanza na la pili wanatakiwa kuwa na leseni C hadi msimu ujao kutakapokuwa na mabadiliko,” alisema Wambura.

 

Aidha, aliongeza kuwa wamevifungia viwanja vya Manungu, Mlandizi na Mwadui ambapo Ruvu Shooting itatumia Uwanja wa JKT Tanzania wa Isamuyo, Mtibwa watatumia Jamhuri na Mwadui watatumia Uwanja wa Kambarage hadi watakapofanyia marekebisho viwanja vyao.

Stori na Khadija Mngwai na Abdulghafal Ally, TUDARCO

TFF Yafanya Mabadiliko ya Mfumo wa Sheria za Ligi

The post Kocha Akivaa Hovyo Uwanjani, Kutimuliwa appeared first on Global Publishers.

No comments: