KMC Waanza Kunona, Wasaini Mkataba wa Bilioni M-Bet
UONGOZI wa KMC inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika umeingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya kubashiri matokeo ya M-bet wenye thamani ya bilioni moja.
Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja Masoko wa M-bet, Allen Mushi alisema; “M-Bet tumeichagua KMC kutokana na namna ambavyo imejipambanua vema katika sekta ya mpira baada ya kupanda daraja ilikuwa ikifanya vema na imeleta ushindani mkubwa.”
Mwenyekiti wa bodi ya KMC, Benjamini Sitta amesema kuwa, M-Bet ni kampuni maalumu ya michezo ya kubashiri na wameingia nao mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya bilioni moja.
Kuelekea kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho dhidi ya AS Kigali ya Rwanda utakaochezwa kesho Uwanja wa Taifa, Kocha Mkuu wa KMC, Jackson Mayanja amesema mchezo utakuwa wa wazi na wamejipanga kupata matokeo chanya licha ya kutokuwa na washambuliaji halisi.
“Kuna baadhi ya majeruhi ambao wapo kwetu jambo linalotuumiza ila hakuna tatizo ni mchezo wetu. “Hatuna mshambuliaji kamili kwa sasa kutokana na majeruhi yanayowasumbua, mchezaji kama Aiyee kwa sasa hayupo sawa ila tumejipanga kufanya vizuri kikubwa sapoti.
The post KMC Waanza Kunona, Wasaini Mkataba wa Bilioni M-Bet appeared first on Global Publishers.
No comments: