Daktari Bingwa Aeleza Sababu Vifo vya Majeruhi wa Moro Kufikia 100

DAKTARI bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Laurian Rwanyuma amesema majeruhi wa ajali ya lori la mafuta iliyotokea eneo la Msamvu mkoani Morogoro wanaendelea kupoteza maisha kutoka na kuungua kwa asilimia 80 hadi 90.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti 21, Dk. Rwanyuma amesema majeruhi wengi waliopelekwa hospitalini hapo, waliungua zaidi sehemu za ndani kama vile mfumo wa hewa na figo hivyo kusababisha kupumua kwa shida.

 

“Kutokana na ngozi zao kuungua kwa asilimia kubwa hali hiyo imesababisha mwili kukosa kinga na kupoteza maji mengi.

“Kwa kawaida wagonjwa walioungua kiasi hicho wana uwezekano mdogo wa kupona hata kama hospitali ina uwezo mkubwa wa vifaa na madawa,” amesema.

 

Hata hivyo, amesema wanaendelea kufanya juhudi za hali ya juu ili majeruhi waliobaki waweze kupona.

Hadi sasa watu 100 katika ajali hiyo ilitokea Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Msamvu mjini Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kulipuka na kusababisha, wamefariki dunia.

The post Daktari Bingwa Aeleza Sababu Vifo vya Majeruhi wa Moro Kufikia 100 appeared first on Global Publishers.

No comments: