JUMUIYA YA WAZAZI CCM KAHAMA YATOA TAMKO KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUWA MWENYEKITI WA SADC

Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga limetoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Tamko hilo limetolewa leo Jumamosi Agosti 24,2019 wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama kilichofanyika katika kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata wilayani Kahama. 

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba, na Katibu wa CCM wilaya ya Kahama,Emmanuel Lameck Mbamange. 

Akisoma tamko hilo,Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) wilaya ya Kahama,Disco Wabare amesema kuchaguliwa kwa rais Magufuli kuongoza SADC inaonesha dhahiri imani waliyonayo viongozi wa SADC kutokana na umahiri na utendaji kazi wake kwa wananchi wa Tanzania na Jumuiya ya SADC. 

"Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa baraza la Wazazi la wilaya ya Kahama kwa pamoja tunatoa tamko la kumpongeza Rais wetu mpendwa,mwenyekiti wa CCM taifa,Amiri Jeshi Mkuu na mtetea wanyonge, Mhe. John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti mpya wa SADC",amesema. 

"Sisi kama Baraza la Wazazi Kahama tunategemea kuona mabadiliko makubwa katika uongozi wake hasa katika kukuza uchumi wa nchi za SADC na kuondoa tatizo la ajira ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa vijana wa nchi hizo",ameongeza Wabare. 

Amebainisha kuwa Baraza la wazazi Kahama linaamini kuwa kwa kasi aliyonayo Magufuli katika kuendeleza nchi ya Tanzania kimaendeleo,ataitumia pia katika kuendeleza umoja wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja aliochaguliwa kuongoza SADC. 

Akizungumza katika kikao hicho,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba alisema pamoja na kumpongeza rais Magufuli ni vyema WanaCCM na Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii. 

Simba ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo mkoani Shinyanga zoezi la Uboreshaji Daftari la Wapiga Kura litaanza Agosti 26,2019 hadi Septemba 1,2019. 

"Tusiishie kujiandikisha tu bali wakati wa uchaguzi ukifika,naomba tukapige kura,ili kuipa ushindi mnono zaidi naomba wanaCCM wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Kila mwanaCCM ajitahidi kuwa na marafiki, wawashiwi wapenzi wa CCM wajitokeze kupiga kura.Tukumbuke kuweka wagombea wanaokubalika kwa kwa wananchi",ameongeza Simba. 

"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni msingi wa uchaguzi mkuu ujao 2020,ili tushinde kwenye chaguzi hizi,ni lazima tushikamane,tuwe na umoja kwani Umoja ni Ushindi.Naomba wingu la makundi liyeyuke,tushikamane,fitna kwetu ni mwiko",amesema Simba. 

Baraza hilo pia limepokea wanachama wapya kutoka vyama vya Upinzani akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) ambaye ameahidi kutoa ushirikiano kuitumikia CCM ili ipate ushindi katika chaguzi mbalimbali zijazo. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama kilichofanyika katika kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata wilayani Kahama leo Jumamosi Agosti 24,2019 .Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Disco Wabare akisoma tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Disco Wabare akimkabidhi wenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akionesha tamko la Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akiwasisitiza wanaCCM kushikamana na kuachana na makundi ndani ya chama. Simba pia aliwataka Makatibu wa CCM kuwapokea wanachama wapya wanaohitaji kujiunga CCM bila kujali kama wametoka vyama vya upinzani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Salim Abdalah Simba akizungumza katika kikao hicho.


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akiwahamasisha wanaCCM kukijenga chama na kukitetea.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akizungumza katika kikao hicho.
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama,Emmanuel Lameck Mbamange akisisitiza kuwa CCM itaendelea kupokea wanachama wapya wanaotaka kujiunga CCM.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama,Sipilaus Bijampola akizungumza katika kikao hicho.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa kutoka wilaya ya Kahama Machimu Mshono Ndalo akiwashukuru wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Kahama kumchagua kuchukua nafasi hiyo licha ya kwamba hakuwepo wakati wa uchaguzi huo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM mkoa wa Shinyanga kutoka wilaya ya Kahama, Greyson Tito Obata Okuku akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kikao kinaendelea.
Kushoto ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akimhamasisha diwani wa kata ya Mwakata,Ibrahim Six kuendelea kufanya kazi ya kuimarisha CCM
Wajumbe wa kikao cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama wakiwa ukumbini.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM wilaya ya Kahama na Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Wigehe, Marco Luswaga Shija akielezea mikakati mbalimbali ya uchaguzi. Shija aliwataka wanaCCM kuweka wagombea wanaokubalika.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) akikabidhi kadi ya CHADEMA na kujiunga CCM leo huku akiahidi kutoa ushirikiano kuitumikia CCM ili ipate ushindi katika chaguzi mbalimbali zijazo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Magung'humwa kata ya Mwakata,Salum Mohammed Salum (CHADEMA) aliyejiunga CCM leo akielezea sababu za kujiunga CCM "Nimerudi CCM kwa sababu sasa kumenoga".
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

No comments: