Ben Pol: Sishindani kula bata

 

KAMA ulikuwa ukijiuliza sana juu ya bata la mkali wa miondoko ya R&B Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ anashindana na nani basi mwenyewe amefunguka kuwa wala hashindani na yeyote.  Ben Pol tangu ameingia katika uhusiano na mpenzi wake ambaye ni raia wa Kenya, Anerlisa, amekuwa akionekana akila bata katika viwanja mbalimbali ikiwemo Marekani, Dubai, Ujerumani, China na Uingereza huku akipiga picha na mastaa wakubwa anaokutana nao.

Akizungumza na Mikito Nusunusu juu ya bata hilo ambalo limezua gumzo mitandaoni kuwa atakuwa anashindana na wasanii wenzake akiwemo Ommy Dimpoz anayefanya kama yeye alisema; “Nimeshawatumikia sana Watanzania na mashabiki wangu hivyo basi ni muda wangu kula bata na sishindani na mtu yeyote.”

The post Ben Pol: Sishindani kula bata appeared first on Global Publishers.

No comments: