OSHA WATAKIWA KUWAJENGEA UWEZO ZAIDI VIONGOZI ILI KUSIMAMIA USALAMA NA AFYA KWA WAFANYAKAZI
Na Khadija seif, Michuzi tv
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Mh Christina Mndeme amewashauri wakuu wa
taasisi mbalimbali kujua vizuri majukumu ya wakala wa usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA) ili waweze kuwasaidia
wananchi kulinda usalama na afya wakiwa kazini.
Mndeme amesema hayo mara baada ya kutembelea Ofisi za Wakala wa
Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) jijini Dar es salaam kujifunza
mambo mbalimbali yanahohusu usalama na Afya kwa Wafanyakazi.
Akizungumza na Uongozi wa Wakala wa usalama na Afya Mahali Pa Kazi
(OSHA) Jiji Dar es salama, Mkuu wa Mkoa huyo alisema Jukumu la Viongozi
wa serikali ni Kuijua OSHA vizuri na kusimamia usalama na Afya sehemu ya
kazi katika maeneo yao.
Alisema yeye kama kiongozi wa Mkoa wa Ruvuma pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, anapokea
Malalamiko kwa watumishi toka sehemu mbalimbali za uzalishaji, hivyo
Kuifahamu vizuri OSHA kutusaidia pia kushughulikia malalamiko yanayoletwa na Wafanyakazi wakiwa maeneo ya kazi.
Hivyo OSHA haina budi kuwajengea uwezo zaidi Viongozi ili waweze kusimamia vizuri usalama na afya kwa wafanyakazi.
Pia Mndeme amewashauri wakala wa usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) kufungua Ofisi zaidi mikoani na kusogeza huduma hizo hadi ngazi ya wilaya jambo ambalo litasadiakufahamika zaidi kwa wananchi wengi na kuwasaidia wananchi walio wengi kwenye maeneo yao.
“Naipongeza serikali kwa kuanzisha OSHA, hivyo niwajibu wetu kuiunga
mkono, kwani shughuli za OSHA zinagusa wananchi wote. Tunajukumu la
kumsaidia Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Katika
kutekeleza majukumu yake, serikali imefanya mengi kupitia serikali ya
awamu ya tano, imeweze kujenga Hospital, kupeleka Umeme hadi Vijijini
hivi sasa kupitia REA wananchi wengi wameweza kuingiziwa
Umeme”alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiwa pamoja na wafanyakazi wa uwakala wa usalama na Afya Mahala pa kazi (OSHA) Mara baada ya kuwatembelea na kupatiwa elimu mbalimbali kuhusu usalama Mahala pa kazi pamoja na majukumu

Dearest Esteems,
ReplyDeleteWe are Offering best Global Financial Service rendered to the general public with maximum satisfaction,maximum risk free. Do not miss this opportunity. Join the most trusted financial institution and secure a legitimate financial empowerment to add meaning to your life/business.
Contact Dr. James Eric Firm via
Email: fastloanoffer34@gmail.com
Whatsapp +918929509036
Best Regards,
Dr. James Eric.
Executive Investment
Consultant./Mediator/Facilitator