Zahera abadilisha upepo Yanga

Mwinyi Zahera raia wa DR Congo

BOSI wa benchi la ufundi la Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amewasisitiza viongozi wa timu hiyo kuwapa mikataba mipya kwa haraka wachezaji waliomo kikosini humo ambao wamemaliza na wapo kwenye malengo yake.

 

Yanga hadi sasa tayari wameshawasajili wachezaji wa timu za nje ambao ni Sadney Urithob, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Lamine Moro, Selemani Mustapha na Abdulaziz Makame.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla amesema; “Kocha Zahera ameagiza kwamba kwa sasa ni kuwabana wachezaji waliopo kwenye timu kwa kuwapa mikataba mipya kwa wale ambao anawahitaji kwa msimu ujao.”

 

“Tayari ameshatoa orodha yake ambapo nalo tutalifanya kama ilivyokuwa kwa wachezaji waliokuwa nje ya timu. Tutamalizana nao na muda siyo mrefu tutaanza kuwatangaza kama ilivyokuwa kwa hawa,” alisema Msolla. SAID

ALLY, Dar es Salaam

The post Zahera abadilisha upepo Yanga appeared first on Global Publishers.

No comments: