WASANII WAOMBA KAMPUNI YA KC LAND KUTENGA MAENEO YA NYUMBA ZA IBADA
Na Khadija seif,Globu ya jamii
WASANII wa Bongo Movie nchini wametoa ombi kwa Kampuni ya KC Land inayouza viwanja kutenga maeneo ya kujenga nyumba za ibada.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na msanii mkongwe wa vichekesho Seif Hassan a.k.a M'bembe ameseam kampuni hiyo inayoshirikiana na kundi la Uzalendo Kwanza bado ina lengo la kumpa heshima msanii kumiliki ardhi kwa manufaa ya kizazi chake.
"Tupo watu wa dini mbalimbali, hivyo ni vema kukatengwa na maeneo ya kujenga nyumba za ibada na lengo kubwa ni kuhakikisha wasanii wanapata nafasi ya kufanya ibada,"amesema.
Hata hivyo M'bembe amewataka wasanii wa kundi la Uzalendo Kwanza kuchukua viwanja, hivyo kwani ni kampuni peke ilionesha dhamira ya dhati ya kuwasaidia wasanii.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya KC Land Khalid Mwinyi amepongeza wasanii wote ambao tayari wameshachukua viwanja na baadhi yao kulipia fedha.
Mwinyi amesema kwa kuwa asilimia 70 tayari wameshalipa , sasa wataweza kukipeshwa fedha kwa ajili ya kununua vifaa ili kuanza ujenzi mara moja.
" Tumefanya hivyo ili kuona kwa jinsi gani mji huu utajengeka kwa haraka zaidi na wasanii kuhamia huku kijiji cha Mwasonga,"
Pia Mwinyi amepongeza watu wa ughaibuni (TDC) kuona ni fursa ya kipekee kuwekeza nyumbani ili kuleta maendeleo nchi ya Tanzania.
"Tayari wameshakatiwa viwanja 200 bado utekelezaji wa kujenga viwanja hivyo na matumaini yangu kutakuwepo na fursa nyingi hasa za kibiashara kutokana na watu hao kuwepo kwenye kijiji hichi hivyo hata huduma za jamii zitakua karibu na wananchi ikiwemo hospital pamoja na nyumba za ibada,"amesema.
No comments: