MUIMBAJI WA KASWIDA INDONESIA ASHAURI WANAWAKE WA KIISLAMU KUPEWA FURSA KUANDAA MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAAN
Na Khadija Seif,Globu ya jamii
MUIMBAJI wa Kaswida kutoka nchini Indonesia Ustadhat Mastia lestaluhu amelipongeza kundi la Nasaha Crew kwa kumpa fursa ya kuja nchini kufanya burudani kwa mashabiki zake walioko nchini Tanzania.
Pia amewahimiza waumini wa dini ya Kiislam hasa waimbaji wa kaswida kuendelea kuwa kwenye misingi ya dini na kutunga Kaswida zenye kuelimisha na kuwakumbusha watu kufanya matendo ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa dini huwaleta wanadamu karibu na ndio maana hata yeye ameweza kutoka nchini kwake na kuja Tanzania, ametoa rai waumini wa dini hiyo kuhakikisha wanapendana na kuiheshimu Quraan Tufuku.
Kwa upande wake Muandaaji wa hafla hiyo fupi ya kusoma Quraan kwa wanawake Ukhty Salama amesema japo kwa sasa wanawake hawajapewa kipaumbele kuanda matamasha na mashindano ya kuhifadhi Quran kupitia hafla hiyo viongozi wataiona nafasi ya kuwaacha wakina mama kuratibu shughuli hiyo.
"Wanawake tunawekwa nyuma sana hasa linapokuja suala la kuratibu vitu vingi ,ila kwa hili la kuandaa mashindano,majukwaa ya kuhifadhi Quraan wanawake wapo tayari kujitoa na kufanikisha hilo,"amesema.
Pia Ukhty salama amewapongeza wanafunzi wake walisoma Quraan Tukufu mbele ya mgeni rasmi Mastia na kueleza ni moja ya nafasi peke ya yeye kubeba mazuri ya nchi yetu nakutangaza sehemu mbalimbali ikiwemo nchini kwake Indonesia.
No comments: