MAANDALIZI YA TAIFA STARS-MISRI
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars,inaendelea vizuri na matayarisho yake kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa michuano ya Mataifa Afrika dhidi ya Senegal,Juni 23 mwaka huu katika Uwanja wa 3o June Cairo.
Kutokana na maandalizi yanayoendelea hadi sasa katika kikosi hicho,benchi la ufundi lina imani kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa ufunguzi na michezo mingine dhidi ya Kenya na Algeria.
Pamoja na wachezaji hao kufanya mazoezi ya uwanjani,pia wamekuwa wanafundishwa mbinu mbalimbali nje ya uwanja kwa kutumia mikanda mbalimbali ya video kuwasoma wapinzani wao,kabla ya kuanza kutupa karata yake rasmi katika mashindano hayo.
Kwa upande wa majeruhi,hadi sasa mchezaji ambaye hatoweza kushiriki mashindano hayo ni Aggrey Morris,ambaye nafasi yake imechukuliwa na David Mwantika,ambaye tayari ashawasili ndani ya kambi tayari kwa ajili ya mashindano.
Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Emmamuel Amuneke,kimeweka kambi nchini Misri tangu Juni 7,kwa ajili ya kuweza kupata nafasi ya kufanya maandalizi ya kina kabla ya kuanza kwa mashindano hayo
TanFootball
No comments: