HAFLA YA KUWAAPISHA WAJUMBE WAPYA WA MABARAZA YA ARDHI YA WILAYA - KAGERA
Anaandika Abdullatif Yunus - Bukoba.
Mkuu Wa Mkoa Wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti amewaapisha Wajumbe wapya wanne Wa Mabaraza ya Ardhi kutoka katika Wilaya za Ngara na Karagwe, katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi mdogo Wa Mikutano Ofisi za Mkuu wa Mkoa mapema Aprili 12, 2019.
Mh. Gaguti amewataka Wajumbe hao kwenda kusimamia Sheria katika misingi ya Haki, huku akisisitiza kuwa Asilimia kubwa ya Migogoro, kesi na kero nyingi ambazo zimemfikia ofisini kwake zinahusiana na masuala ya Ardhi. Hivyo kupitia uteuzi wao ni vyema kuzingatia Maadili ya kazi yao, na kujiepusha masuala yanayoweza kupindisha haki ikiwemo Rushwa.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Bukoba Lucia Kairo, amewataka wajumbe hao kuwa waaminifu, na kutumia weledi katika kazi zao za kuyasaidia mabaraza ya Ardhi.
Wajumbe hao wapya walioapishwa ni Ndg. Longino Frederick (Wilaya Karagwe), Lucletia Shubilo (Wilaya Karagwe), Christina Mugasha (Wilaya Ngara), na Charles Mbeikya (Wilaya Ngara).
Kupitia Hafla hiyo pia Mkuu wa Mkoa Mh. Gaguti amewatambulisha Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Kanda Bukoba, ambao wameongezwa katika mahakama hiyo.
Pichani ni Ndg. Longino Mbeikya Mjumbe mteule wa Baraza la Ardhi Wilaya Karagwe akila kiapo Mbele ya Mkuu wa Mkoa Kagera Mh. Gaguti.
Pichani ni Bi. Christina Mugasha Mjumbe mteule wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Ngara akila kiapo Mbele ya Mh. Gaguti, Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika hafla ya Kuwaapisha Wajumbe hao.
Pichani ni Ndg. Lucletia Shubilo Mjumbe mteule wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Karagwe akila kiapo Mbele ya Mh. Gaguti Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Pichani ni Ndg. Charles Mbeikya Mjumbe mteule wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Ngara, Mara baada ya kula kiapo, akiwa amesimama Mbele ya Mh. Gaguti, Mkuu wa Mkoa Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza na Wajumbe wapya wa Mabaraza ya Wilaya (hawapo pichani) pamoja na wananchi Mara baada ya Kuwaapisha.
Sheikh wa Mkoa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta akitoa neno na Dua katika hafla ya Kuwaapisha Wajumbe wapya wa Mabaraza ya ardhi ya Wilaya
Mchungaji King James wa Hema la Ukombozi akitoa maombi yake katika hafla ya Kuwaapisha Wajumbe wa Mabaraza la Ardhi ya Wilaya za Karagwe na Ngara.
Sehemu ya Wajumbe na wageni waalikwa wa Hafla fupi ya Kuwaapisha Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya za Ngara na Karagwe katika ukumbi mdogo wa Mikutano Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera.
Picha ya Pamoja Mara baada ya hafla ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Mabaraza ya Ardhi ya Ngara na Karagwe.
No comments: