Wawa awa kivutio Arusha
BEKI kisiki wa Simba, Pascal Wawa, jana alikuwa kivutio kwa mashabiki wa soka wa jijini hapa waliojitokeza kushuhudia mchezo wa Ligi kuu Bara kati ya African Lyon na Simba kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Wawa raia wa Ivory Coast, alikuwa kivutio wakati wachezaji wa Simba walipoingia uwanjani hapo majira ya saa 8 mchana kabla ya kuanza kwa mchezo wenyewe saa 10 jioni.
Licha ya Simba kuwa na nyota wengi, lakini mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo walionekana kumshangilia zaidi Wawa huku naye akionyesha kufurahishwa na jambo hilo.
Mara baada ya wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kuingia vyumbani, kocha wa kikosi hicho, Patrick Aussems alitoka na kwenda kukagua sehemu ya kucheza, kisha akarudi tena vyumbani na kujiridhisha kwamba uwanja upo katika hali nzuri.
The post Wawa awa kivutio Arusha appeared first on Global Publishers.
No comments: