Jerry Muro Avaa Jezi Ya Simba, Atambiana Na Manara – Video

ALIYEKUWA Ofisa Habari wa Yanga ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, jana walitambiana kati ya Simba na Yanga, timu gani itakuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Tukio lilitokea wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya African Lyon dhidi ya Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.

 

Championi lilimshuhudia Muro akifika uwanjani hapo na kwenda kukaa jukwaa la waandishi wa habari ambalo lipo karibu na jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo mashabiki wa Simba wakamnunulia jezi ya Simba wakitaka aivae.

 

Kabla ya Muro kuivaa jezi hiyo, alimuomba Manara ndiyo aivae, lakini baadaye akaivaa na kuanza kutambiana huku Muro akisema msimu huu Yanga inakuwa bingwa, wakati Manara anasema Simba itakuwa bingwa.

 

Manara alifikia mbali na kumwambia Muro ataje jina la Kagere ili ampatie Sh 50,000, lakini Muro aligoma na kusema: “Arumeru yote kuna Yanga na Simba, mimi kuvaa jezi ya Simba si tatizo, lakini niwaambie Simba kuwa ubingwa msimu huu ni wa Yanga.”

The post Jerry Muro Avaa Jezi Ya Simba, Atambiana Na Manara – Video appeared first on Global Publishers.

No comments: