MAHAKAMA YATENGUA WAJUMBE WA LIPUMBA, YAIFUTA BODI YAKE

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, leo Jumatatu Februari 18, 2019, imetengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama Cha Wananchi (CUF) wa kambi ya Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

 

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Dk Benhajj Masoud baada ya kubatilisha uteuzi wao, amesema majina yaliyokuwa yamependekezwa na kambi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, hawakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa bodi hiyo, hivyo nao hawakuwa wamekidhi matakwa ya sheria.

 

Wakili wa CUF  kambi ya Maalim Seif, Juma Nassoro amesema wajumbe wa bodi waliokuwepo wanaendelea na majukumu yao licha ya kwamba muda wao umeshaisha hadi hapo wajumbe wengine watakapoteuliwa.

 

Katika kesi ya Msingi, Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Saleh alifungua kesi hiyo akipinga uamuzi wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita) wa kuwaidhinisha wajumbe waliopendekezwa na kambi ya Profesa Lipumba kuwa wajumbe wapya wa bodi hiyo.

 

BREAKING | MAALIM SEIF AKIZUNGUMZA

The post MAHAKAMA YATENGUA WAJUMBE WA LIPUMBA, YAIFUTA BODI YAKE appeared first on Global Publishers.

No comments: