Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual yawanoa mawakala kwa stadi mpya za biashara
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Kukuza Biashara wa UAP Old Mutual Insurance Jabir Kigoda akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya mawakala yaliyoandaliwa kwa ajili ya mawakala wa kampuni hiyo hivi majuzi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mawakala wa UAP Old Mutual Insurance wakifuatilia mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es salaam hivi majuzi.
Meneja wa Kukuza Biashara wa Old Mutual Insurance , Charles Magori, akiwasilisha mada katika mafunzo kwa mawakala wa kampuni hiyo Dar es Salaam hivi majuzi.
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya bima ya Old Mutual Insurance hivi majuzi waliendesha mafunzo ya siku moja kwa mawakala wake ambayo ililenga kuwanoa katika stadi mpya za biashara katika sekta hiyo inayokuwa kwa kasi.
Mfunzo hayo, yaliyohudhuriwa na mawakala 60 wa kampuni hiyo kutka maeneo mabalimbali ilijikita katika kuwapa mawakala stadi mpya katika Nyanja mbalimbali kuanzia bidhaa, mauzo na kanuni mbalimbali za uendeshaji.
“ Mafunzo ya aina hii vilevile yanantoa fursa ya kuwasiliana ana kwa ana na mawakala ambayo ni njia rafiki . Isitoshe, mawakala wanapata fursa ya kutambua maswala mbalimbali yanayojitokeza mara kwa mara katika soko la bima kwa ujumla,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Kukuza Biashara wa UAP Jabir Kigoda, alipokuwa akifafanua dhana ya mafunzo hayo.
Kati ya maeneo yaliyoguswa na mafunzo hayo ni namna ya kukidhi matakwa ya sheria mbalimbali za udhibiti biashara ya bima, kitu ambacho ni muhimu kuwezesha mawakala kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria zilizopo. “ Hii itasaidia sana kuhakikisha kuwa mawakala hawavunji sheria na hivyo kuondoa mikwaruzano isiyo ya lazima na vyombo vya sheria, kanuni na taratibu,” alisema Kigoda.
Akifafanua kwa jinsi mafunzo hayo yalivyoendana na wakati, Kigoda alisema “ Mafunzo haya yamekuja katika muda muafaka kwa kuwa azma yetu daima ni kuwapa wateja wetu huduma bora. Nina uhakika yatasaidia kwa kiwango kikubwa kuwafanya mawakala kutambua namna ya kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi kwa siku za usoni .”
No comments: