CHID BENZ, “USIHUKUMU KITABU KWA KUTAZAMA KAVA LAKE”

Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.

KUNA msemo wa Kingereza usemao; “Don’t judge a book by it’s cover”. Zipo tafsiri zisizo za moja kwa moja za Kiswahili kwamba; “Usihukumu kitabu kwa kuangalia mwonekano wake wa nje”.

 

Na tafsiri zaidi ni kwamba usimchukulie poa mtu alivyo kwa nje bila kujua ndani yake kuna nini. Na usichukulie sifa mbaya ya mtu na kuamini ndivyo alivyo. Ukifanya hivyo unakosea sana!  

 

Hilo linathibitishwa na rapa bora kabisa kuwahi kutokea kwenye muziki huu wa Bongo, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’. Miongoni mwa mambo yaliyotrendi wikiendi iliyopita ni kauli za Chid. Alikuwa akihojiwa na televisheni moja ya mtandaoni. Baada ya intavyu ile, Chid akageuka gumzo.

 

Kwani Chid huyuhuyu ambaye watu wanachu kulia poa alisema? Alitoa kauli ambazo wengi wa watu waliomsikiliza waliishia kusema; “Kumbe huyu jamaa ana akili sana” na “kumbe inawezekana madawa ya kulevya yanaathiri tu mwili tu na siyo akili”. Mbali na kuchana sana na kuthibitisha kuwa ndiye mfalme wa freestyle aliyebaki baada ya kifo cha Ngwea na Godzilla, Chid alifunguka mambo makubwa yaliyosababisha gumzo;

 

Chid alikuwa akijibu swali kama anajua kwamba kuna bilioni mbili za wasanii zilizotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (Pichani) ambapo majibu yake yalikuwa ni haya;

 

“Aliniambia mama yangu. Unajua huwa sifuatilii sana TV. Nikamwa mbia sawa ngoja niende. Lakini sielewi Makonda anafanya nini, lakini mimi ni rafiki yangu mzuri sana. “Lakini ninamshauri ange-relax, afanye vitu vichache kwanza avikamilishe, vile ambavyo vimemuweka kwenye kile kiti anachokalia now (sasa) kuliko ku-mix muziki, michezo, nini na nini na Serikali, kutamchanganya.

“Na hata akijaribu kufanya vyote akihisi nguvu hiyo anayo, sidhani kama nguvu hiyo anayo kwa sababu pale ofisini kwake ninapajua, nimeishi pale yaani ni opposite (mkabala) na kwangu kwa hiyo ninawajua wote waliokaa pale.

 

“Makonda anajitahidi sana, lakini asifanye vitu ambavyo baadaye vitampa lawama. Unajua watu wengine wanakusubiri ukishamaliza ule muda wako ndipo wanaanza kukupa lawama. “Ni suala zuri (mikopo kwa wasanii) aliloliamua, lakini asi-base (asiegemee) sana kwa wasanii, watu wa michezo, muvi… no…no… nooo…

 

“Ange-stick (angesimama) kwenye masuala ya kuondoa watu pale Kariakoo, magari yapite vizuri. Ange-stick kwenye mitumba maana watu wanajua Karume, lakini watu hawapapendi, ange-stick pale ajue mabanda yanafanywaje, kule ndani kungekuwa na mashine ya pesa (ya kukusanya ushuru) ili mtu akiuza mtumba kwa Wakongo au Wamalawi wengi wanakuja na pesa nyingi hawawezi kutembea nazo hivyo angehakikisha kuna hizo mashine. “Pia angefanya utaratibu wa mahospitalini madawa yawepo sana, kusiwe kuna complain (malalamiko) ya aina yoyote.

 

“Pia angefanya uwezekano wa vituo vya daladala vijengwe labda kiaina f’lani (kisasa), viwe na sehemu ambayo mtu akikaa jua lisimpige. Angekuwa anadili na vitu fulani vikubwa vya nchi tungesema tunaweza kumsapoti na kumshangilia zaidi kuliko kuja kudili na watu wa michezo na muziki akiamini kwamba tunaweza tukapiga kelele zaidi ya kumsifia, lakini sisi (wasanii) dakika ya mwisho huwa tunataka tu utupe hela.

 

Sisi mtu hata akiwa na plan (mpango) mingi huwa tunachotaka ni hela tu. Sasa kama hela haitoki, watu watarudi upande wako wa pili kuangalia umefanya lipi la maana?”

 

Ukiacha suala hilo, Chid alifunguka juu ya vifo vya wasanii akiwataka kuwa makini mno hasa katika kipindi hiki kwani zamani wao waliinjoi kufanya muziki, lakini sasa inabidi mtu uchague kuwa msafi au mchafu. Uwe msafi uinjoi au mchafu upotee! Kufuatia intavyu hiyo na mwonekano ‘smart’ wa Chid, wapo walioamini amerudi vizuri kwenye gemu!

The post CHID BENZ, “USIHUKUMU KITABU KWA KUTAZAMA KAVA LAKE” appeared first on Global Publishers.

No comments: