TAARIFA MUHIMU KUTOKA UONGOZI WA KLABU YA SIMBA

Uongozi wa Klabu ya Simba unapenda kuwataarifu wanachama, wapenzi na mashabiki wake kuwa mchana wa leo baada ya Sala ya Ijumaa (Saa 8.00) kutakuwa na KISOMO katika Makao Makuu ya Klabu Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Lengo la KISOMO hiki ni kumuomba Mwenyezi Mungu aweze kuleta wepesi kwenye matatizo yaliyompata Mlezi na Mwekezaji wetu Bw. Mohammed Dewji “MO”

Tunapenda kuwakaribisha katika Kisomo hiki muhimu ili kumuomba Mungu aweze kumlinda na kumrejesha Mwenzetu salama.

Tunatanguliza Shukrani.

The post TAARIFA MUHIMU KUTOKA UONGOZI WA KLABU YA SIMBA appeared first on Global Publishers.

No comments: