JIDE KUMSHUSHA JULIANA WA UGANDA DAR

Image result for lady jay dee

Judith Wambura Mbibo, ‘Lady Jaydee’

KWA mara ya kwanza katika Muziki wa Bongo Fleva, mkongwe wa muziki huo, Judith Wambura Mbibo, ‘Lady Jaydee’ anatarajiwa kumshusha mkali wa muziki kutoka Uganda, Juliana Kanyomozi katika onyesho liitwalo Vocals Night, litakalofanyika Oktoba 26 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Showbiz, Lady Jaydee ambaye pia ni maarufu kama Jide, alisema katika onyesho hilo, pia atakuwepo msanii kutoka Afrika Kusini, Zahara Bulelwa Mkutukana na wasanii wawili wa nyumbani, Damian Soul na Grace Matata.

 

“Nina ndoto ya kulifanya onyesho hili kuwa ni la kila mwaka na lango lake kubwa ni kutaka kuwakomboa wasanii wanawake ambao wengine wanalazimika kuuza utu wao ili wafanikiwe katika kazi zao, maana kama unavyojua wanaume wameishika hii sanaa karibu kila sehemu.

 

Image result for Juliana Kanyomozi

“Kama mtu hayuko tayari kutoa rushwa ya ngono inakuwa ni vigumu kupenya katika soko, lakini mimi nataka niwe daraja lao. Ndiyo maana nimemchukua msanii kama Grace, anafanya kazi nzuri lakini hasikiki,” alisema Jide.

 

Msanii huyo ambaye ameendelea kubakia katika ubora wa juu kimuziki licha ya changamoto nyingi zilizowafanya wenzake wengi alioanza nao kutoweka, alisema katika onyesho hilo, anataraji pia kutoa zawadi ya nyimbo yake mpya ambayo ataitoa hivi karibuni.

 

Katika kunogesha onyesho hilo ambalo kiingilio chake kitakuwa ni shilingi elfu 25 kwa mashabiki wa kawaida, 50,000 kwa watu maalum na 150,000 kwa walio maalum zaidi, mshereheshaji wa tukio hilo anatarajiwa kuwa Uti Nwachukwu, ambaye ni mmoja wa washiriki wa Big Brother 5 All Stars mwaka 2010 ambaye alidumu kwa siku 91.

 

“Uti pia ni muigizaji kule kwao Nigeria, na nimemleta mahsusi ili kuchanganya ladha katika tukio hilo ambalo ninategemea kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wangu ambao siku zote wamek-uwa samb-amba na mimi, kiasi cha kunipa faraja kwel-ikweli,” alisema Jide.

The post JIDE KUMSHUSHA JULIANA WA UGANDA DAR appeared first on Global Publishers.

No comments: