Waziri Mwakyembe atoa fursa kwa vijana waliyomaliza Shahada kupata mafunzo ya ualimu wa lugha Kiswahili kwa Wageni

Na Anitha Jonas – WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana wote wa kitanzania waliohitimu Shahada katika vyuo vikuu nchini kujitokeza na kwenda Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa ajili ya kupata mafunzo yatakayowasaidia  kuwa walimu wa lugha ya Kiswahili kwa wageni kutokana na wataalamu wa lugha hiyo kusuasua kujiandikisha katika kanzi data ya wataalamu wa hiyo.  
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga mafunzo ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili yaliyoandaliwa na BAKITA kwa ajili ya kuwajengea Ustadi wataalamu ya Kiswahili ili waweze kufundisha wageni lugha ya  Kiswahili. 
“Mpaka sasa nimepewa takwimu za  wataalamu  tisini na sita  wa lugha ya Kiswahili nchini  ambao ndiyo waliyojitokeza  waliyojitokeza kujiandikaisha katika kanzi Data ya waatalamu wa lugha hii,kwa kweli sijui ni kwanini watanzania wanakuwa wazito katika kuchangamkika fursa badala yake mambo yakibadilika wataanza kulalamika,kwani lengo la kanzi data hii ni kurahisisha mfumo wa kuwafikia wataalamu wa lugha hii kwa haraka pale fursa zinapo kuja,”alisema Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika sherehe za kufunga mafunzo hayo Waziri huyo mwenye dhamana na masuala ya lugha nchini alieleza kuwa kwa sasa kuna uhitaji mkubwa wa wataalamu kwa ajili ya kufundisha lugha ya Kiswahili na tayari kuna maombi yamesha kwisha wakilishwa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Sudani Kusini, Rwanda na Afrika ya Kusini kwajili ya kupatiwa waatalamu wa lugha ya Kiswahili na wataokweda kufundisha katika nchini hizo.
Kwa upande wa Katibu Mtendaji BAKITA Dkt.Selemani Sewangi alimpongeza mheshimiwa Waziri Mwakyembe na kumweleza kuwa taasisi hiyo hivi karibuni inatarajia kuanza kutoa mafunzo ya ukalimani na wanatoa wito kwa watanzania wote na wataalamu wa lugha wanaoona kuwa wanauwezo wa kuwa wakalimani wa lugha mbalimbali wafike  katika ofisi yao kwa ajili ya kupata mafunzo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati)akizungumza na wahitimu wa mafunzo ualimu wa lugha ya Kiswahili kwa wageni yaliyokuwa yanatolewa na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) leo Jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kuwakabidhi vyeti wahitimu wa mafunzo hayo,kutoka kulia ni Katibu Mtendaji BAKITA Dkt.Selemani Sewangi.
 Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Tanzania Dkt.Selemani Sewangi (kulia) akimweleza Mheshimiwa  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison mwakyembe mchakato wa taasisi hiyo wa kuanzisha programu ya mafunzo ya ukalimani hivi karibuni leo jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe ya kuwakabidhi vyeti walimu  wa lugha ya Kiswahili kwa wageni baada ya kumaliza mafunzo yao.
Mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya ualimu wa Lugha ya Kiswahili kwa wageni ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na mwanafunzi wa PHD katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mwl.Editha Adolf akisoma shairi la kusifu lugha ya Kiswahili mbele ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) katika sherehe ya kuwa kabidhi vyeti wahitimu  hao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi cheti Mwalimu Prisca Mihayo kutoka Shule ya Sekondari Meli  Mkoa wa Kilimanjaro leo jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ualimu wa lugha ya Kiswahili kwa wageni yaliyokuwa yanatolewa na Baraza la Kiswahili la Tanzania. 
 Waziri wa Habari Utamdauni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya ualimu wa lugha ya Kiswahili kwa wageni mara baada ya kuwakabidhi vyeti vyao vya kuhitimu mafunzo hayo yaliyokuwa yanatolewa na Baraza la Kiswahili Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

No comments: