TAXIFY YAZINDUA HUDUMA ZAKE JIJINI DODOMA
Huduma ya teknoloJia ya teksi inayoongoza Ulaya na Afrika ya Taxify leo imezinduliwa jijini Dodoma na mamia ya madereva teksi ambao wamesajiliwa na Taxify wameanza kutoa huduma kwa wananchi.
Huduma ya Taxify mjini Dodoma itatoa njia salama na ya bei nafuu kwa abiria kupata usafarishaji na usalama wa wateja umeongezeka kwa kutumia teknolojia ya “Share your ETA“ ambayo inampatia mteja fursa ya kutaarifu familia na marafiki safari yake na kuwahakikishia usalama wake.
Menjea Mkuu Tanzania Remmy Eseka amesema: "Baada ya kuzindua huduma yetu jijini Dar es Salaam na Mwanza, tunaendelea kupanua wigo wa huduma, na mji mkuu wa Dodoma ni mojawapo ya miji ya msingi katika soko letu. Tuna imani ya kwamba watanzania watanufaika na huduma zetu.”
Taxify imetua Dodoma na ofa mbalimbali ambazo zimelengwa kunufaisha madereva ambao wamejisajili na huduma yao.
Kampuni imetoa mikopo ya simu za kisasa za kiganjani zitakazowawezesha madereva kujiunga na tukutmia teknologia hii katika kutoa huduma kwa wateja.
Katika hili madereva wamepatiwa fursa ya kulipia kwa awamu ya mwezi kwa mwezi kutokana na faida watakayopata kwenye biashara.
Aidha kampuni imeshirikiana na kampuni ya mafuta ya Total na kutoa punguzo la bei ya mafuta na bidhaa za Total kwa madereva wote ambao watajiunga na kadi ya Total.
"Tunafurahia kuwa wa kwanza kutoa huduma ya teknologia ya texsi mjini Dodoma na kuunganisha madereva mbalimbali na huduma yetu. Tuna uhakika teknologia yetu italeta urahisi na kupunguza ucheleshewaji wa kutoa huduma katika jijini,” alisema Shivachi Muleji, Meneja Mkuu wa Afrika Mashariki.
Pia, kampuni imelenga kuwanufaisha madereva kwa kutoza ada ndogo ya kutumia teknologia yao kwa asilimia 15 tu, ambayo ni zaidi ya nusu ya ada wa washindani wao nchini na kote duniani.
"Daima tunatafuta ushirikiano na fursa ambazo zitawezesha madereva kupata faida kubwa zaidi kwa kupunguza gharama za kufanya biashara. Tunaamini kwamba madereva watafurahia kazi yao na kutoa huduma bora kwa wasafirishaji. Madereva tulionao wamefurahishwa na punguzo la gharama ya mafuta kwa kuwa punguzo ni la hapo papo kwenye pampu," alisema Remmy Eseka
Kampuni ya taxify imeweka mipango ya kupanua wigo wa huduma katika Afrika Mashariki na inayomikakati ya kuleta huduma yao kwa madereva bajaji na pikipiki.
Menjea Mkuu Tanzania Remmy Eseka akizunggumza na waandishi wahabari wakati wa uzinduzi wa huduma zake katika Jiji la Dodoma.
No comments: