Siwezi Kumzungumzia Sister Fey, Hakuwahi Kufundisha cha Maana Katika Jamii :-Steve Nyerere
Msanii wa bongo movies Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa hawezi kukaa katika vyombo vya habari na kuanza kumzungumzia Sister Fey kwa sababu kufanya hivyo ni kujidharirisha yeye mwenyewe kwa sababu Sister Fey hama cha muhimu cha kumzungumzia.
Akiongea na mwandishi wa habari Steve Nyerere anasema kumzungumzia Sister Fey ni sawa na kujidharirisha yeye kwa sababu unapomzungumzia steve nyerere unazungumzia nchi hivyo ni sawa na nchi kushindana na kijiji.
Hata hivyo Steve anasema kuwa kutokana na mambo mabaya aliykuwa akiyafanya Sister Fey likiwemo la kujiingiza katika mahusiano na mtoto mdogo limefanya hakuna hata msanii mmoja anaetaka kujua anaendeleaje huko alipokamatwa kwa sababu hiyo ilikuwa ni utovu wa nidhamu.
Lakini pia Steve anasema kuwa hii sio kawaida kwa msanii hata mmoja kutokumkumbuka sister fey lakini kutokana na mabaya yake ndio maana hakuna anaetaka kujua habari zake na kwa upande wake yeye anaona ni sawa tu kukamatwa kwake.
The post Siwezi Kumzungumzia Sister Fey, Hakuwahi Kufundisha cha Maana Katika Jamii :-Steve Nyerere appeared first on Ghafla!Tanzania.
No comments: