PROFESA MBARAWA ATOA ONYO KWA MKANDARASI MWESE

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ametoa onyo kwa Kampuni ya Monmars & Sons Ltd kutokana na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Mwese uliopo wilayani Tanganyika (zamani Mpanda Vijijini) mara baada ya kutembelea mradi huo mkoani Katavi.

Profesa Mbarawa amemuonya mkandarasi anayefanya kazi hiyo na kumtaka aongeze kasi ya utekelezaji, vinginevyo itamlazimu kuchukua maamuzi magumu kwake.Profesa Mbarawa amesema amefika Chamalendi na kukuta mradi mwingine unaotekelezwa na mkandarasi huyo unasuasua, kama ilivyo Mwese na kumtaka ajirekebishe.

“Nakupa nafasi ujirekebishe na kumaliza kazi hii na kazi nyingine zote za miradi ya maji ulizonazo, ukishindwa itanilazimu kukuchukulia hatua”, ameagiza Profesa Mbarawa.Mbunge wa Jimbo la Tanganyika (zamani Mpanda Vijijini), Moshi Kakoso amemshukuru Profesa Mbarawa kwa ufuatiliaji wake wa miradi ya maji, hususani katika mkoa wa Katavi na kusema kuwa kwa kazi kubwa anayoifanya sekta hiyo itapiga hatua kubwa kimaendeleo.

“Nakushukuru sana Waziri wa Maji kwa kazi yako nzuri ya ufuatiliaji wa miradi ya Serikali, kwa utendaji wako sina mashaka kufikia mwaka 2020 malengo ya sekta hii yatafikiwa”, alisema Kakoso.Profesa Mbarawa amemaliza ziara yake yake ya kikazi mkoa wa Katavi kwa kutembelea wilaya zake zote za Mpanda Mjini, Mlele na Tanganyika
Ujenzi wa tenki la maji mradi wa Mwese ukiwa kwenye hatua za awali.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa tenki la maji mradi wa Mwese uliopo katika Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi.
Mkandarasi akipima ubora wa matofali ya ujenzi mbele ya Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mbunge wa Jimbo la Tanganyika (zamani Mpanda Vijijini), Moshi Kakoso wakielekea kwenye chanzo cha maji cha mradi wa Mwese.
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na msafara aliongozana nao wakikagua chanzo cha maji cha mradi wa Mwese.

No comments: