Khadija Kopa Afungukia Skendo Ya Kifumaniwa
Mwanamuziki wa Taaprabu nchini Khadija Kopa au Malkia wa Mipasho amefungukia skendo iliyowahi kumtafuna miaka ya nyuma kwamba moja kati ya ndoa zake nne ilivunjika baada ya fumanizi.
Katika mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo ya EA radio, Khadija amesema pamoja na kwamba miaka hiyo hakukuwa na mitandao ya kijamii lakini vyombo vya habari vilitengeneza stori kama hizo ili viweze kuuza gazeti:
Skendo ambayo niliwahi kuwa nayo kubwa miaka hiyo ni kutangazwa kuwa nimeachwa kwa kile walichodai kuwa nilifumaniwa. Ila kiukweli sijawahi kufumaniwa ila ni watu walizusha ili kusudi ya kwao yawaendee vizuri si unajua miaka hiyo hakukuwa mitandao ya kijamii kama ilivyo hivi sasa”.
Khadija ameweka wazi siri yake ya kuendelea katika tasnia ya Muziki wa taarabu ni kubadilika kutokana na mazingira na mashabiki ili kuendelea kuwapa ladha tofauti tofauti.
The post Khadija Kopa Afungukia Skendo Ya Kifumaniwa appeared first on Ghafla!Tanzania.
No comments: