Country Boy Athibitisha Kuzika Bifu Lake na Mama Watoto Wake

Msanii wa Hip Hop  anayetamba kwa kibao cha cha ‘Wanaona haya’ Country Boy amethibitusha kumaliza mvutano uliokuwepo baina yake na kama watoto wake.

Country Boy amethibitisha kuwa baada ya bifu hilo kuisha yeyye na mama watoto wake wamejikuta katika nafasi nzuri zaidi na kwa sasa ni ruksa kumuona tena mtoto wake ‘Rakim’.

Country Boy na Baby mama wake walivurugana kisa matunzo ya mtoto ambapo Mwanamke huyo alimtuhumu Msanii huyo kwa kutotoa matunzo ya mtoto.

Katika Interview aliyofanya na kituo kimoja cha habari hivi karibuni, Country Boy amesema masuala yaliyokuwa yakiendelea baina yake na mzazi mwenzake ni ya kawaida na mtu yeyote yanaweza kumtokea kwenye jamii ya sasa.

Siwezi kujua kwamba ni kwa nini aliamua kuongea alichokiongea kwenye mitandao ya kijamii pamoja na ‘media’, lakini naamini kwamba yupo sawa na kila kitu ambacho amekiongea huenda aliongea akiwa na hasira. Pia katika hali ya kawaida naamini kanielewa kwamba mimi ni binadamu na mpaka sasa tunaongea vizuri na tunapiga stori kama kawaida”.

Kwenye Interview alizofanya na vituo vya habari Mwanamke huyo pia alimtuhumu Country Boy kwa kuvuta Bongo mbele ya mtoto wao.

The post Country Boy Athibitisha Kuzika Bifu Lake na Mama Watoto Wake appeared first on Ghafla!Tanzania.

No comments: