ASASI ZA KIRAIA ZINAZOJIHUSISHA NA UTAWALA BORA MKOA WA DODOMA ZAPATIWA MAFUNZO KUHUSU SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Katibu Msaidizi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ofisi ya Kanda ya Kati Dodoma, Bw. Cathlex Makawia (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ya Maadili kwa Asasi za Kiraia zinazojishughulisha na Utawala Bora, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga iliyoko Jijini Domama Septemba 25, 2015. Lengo ya Mafunzo hayo ni kuzijengea uwezo Asasi za Kiraia kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya mwaka 1995 ili zikaweze kusimamia na kukuza maadili ya viongozi kwa Jamii.
Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kaskazini Arusha, Bibi. Anna Mbasha akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 kwa wawakilishi wa Asasi za Kiraia zinazojihusisha na Utawala Bora Mkoani Dodoma leo Septemba 25, 2018 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga.
Mshiriki wa Mafunzo ya Maadili kwa Asasi za Kiraia zinazojihusisha na Utawala Bora Mkoa wa Dodoma, Bw. Aggrey Mbassaga kutoka Asasi ya SWORD akiuliza swali kutokana na Mada iliyokuwa imewasilishwa kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya Mwaka 1995.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Maadili kutoka Asasi za Kiraia zinazojihusisha na Utawala Bora Mkoani Dodoma, wakifutilia mada iliyokuwa inawasilishwa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bibi. Anna Mbasha (hayupo kwenye picha) Septemba 25, 2018 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga iliyopo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Maadili kutoka Asasi za Kiraia zinazojihusisha na Utawala Bora Mkoani Dodoma, wakifutilia mada iliyokuwa inawasilishwa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bibi. Anna Mbasha (hayupo kwenye picha) Septemba 25, 2018 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga iliyopo Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo ya Maadili kwa Asasi za Kiraia zinazojihusisha na Utawala Bora Mkoani Dodoma. Waliokaa kutoka kulia ni Afisa wa Sekretarieti ya Maadili Kanda ya Kaskazini, Bw. Musiba Magoma, Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,Ofisi ya Kanda ya Kati Dodoma Bw. Cathlex Makawia akifuatiwa na Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Bibi. Anna Mbasha.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa DIPEDEA, Bw. Hassan Hussein.
No comments: